Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Msanii Mrisho Mpoto amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kutumia ukali kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu mbele ya Rais Samia na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea Ripoti ya Utafiti wa Afya ya uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria na Ugawaji wa Magari ya kubebea wagonjwa.
Msanii huyo akitumbuiza amesema hataki kusikia stori za COVID ama vita ya Ukraine ndio vimesababisha kupokea magari pungufu bali stori pekee wanayotaka kuisikia ni kuwa magari yote yaliyokusudiwa yamefika.
Wageni waalikwa, inabidi mkae kwa umakini mkisikia Mrisho Mpoto yumo kwenye orodha ya watumbuizaji, naona ameshika kasi na hakuna wa kumzuia.