Kwa kweli katika hili Mpoto alipoteza uzalendo na alitutoa katika ramani ya dunia. Binafsi namweshimu sana Mpoto ila niliposikia habari zile kwa mara ya kwanza niliumia mno!
Kama kweli alikuwa mzalendo na mzawa angestop pale pale penye uongo wa kusaliti Tz, naamini hata wazungu WANGEMHESHIMU sana kwani hakuna kitu chaweza shinda uzalendo. Dunia nzima ingesimama kwa muda na hata vyombo vikubwa kabisa vya media duniani vingeripoti tukio lile na dunia ingejua sasa kuwa hizo ni hujuma za Kenya na sasa ukweli ungekuwa wazi na watu kibao wangependa kuja Tz kujiknea ukweli. Nimeumia sana na hakika pesa ni mwanaharamu!