Hongera mjomba,kama kweli hukuonekana kutumika kama daraja!
Heshima yako itabakia kuwa juu daima,maana umekwepa meno ya wanasiasa kukutafuna kama muwa na mwisho kukutema ptuuuu!
Njaa mbaya,njaa yaweza kusababisha utu kupotea,wangapi wameuza utu wao ili tu mkono uende kinywani?
Kahaba huonyesha kumpenda kila mteja wake ilimradi tu baada ya huduma atampa chochote kitu ili maisha yaende,ingawa moyo walia machozi!
Kuuza utu sababu ya pesa ni kitu kbaya sana,hasa pale unapouza utu wako kwa mtu ambaye unajua kabisa anakutumia kutimiza haja au shida zake na hana mapenzi ya kweli kwako.
Hongera mjomba,maana macho yangu ya makengeza hayajakuona ukipwayuka katika majukwaa ya kisiasa,yaani ukitumika kama kiishacho radha,ambapo mwisho wa kampeni ukatupwa kama taka katika jalala!
Bora utu,kuliko fedha zenye kudharirisha utu!
Umeitunza heshima yako;daima mashairi yako yatakua na thamani zaidi ya dahabu