Mrisho mpoto Hongera,sijakuona katika majukwaa ya kampeni za kisiasa 2015

nyuli

Senior Member
Joined
Sep 7, 2012
Posts
128
Reaction score
95
Hongera mjomba,kama kweli hukuonekana kutumika kama daraja!

Heshima yako itabakia kuwa juu daima,maana umekwepa meno ya wanasiasa kukutafuna kama muwa na mwisho kukutema ptuuuu!

Njaa mbaya,njaa yaweza kusababisha utu kupotea,wangapi wameuza utu wao ili tu mkono uende kinywani?

Kahaba huonyesha kumpenda kila mteja wake ilimradi tu baada ya huduma atampa chochote kitu ili maisha yaende,ingawa moyo walia machozi!

Kuuza utu sababu ya pesa ni kitu kbaya sana,hasa pale unapouza utu wako kwa mtu ambaye unajua kabisa anakutumia kutimiza haja au shida zake na hana mapenzi ya kweli kwako.

Hongera mjomba,maana macho yangu ya makengeza hayajakuona ukipwayuka katika majukwaa ya kisiasa,yaani ukitumika kama kiishacho radha,ambapo mwisho wa kampeni ukatupwa kama taka katika jalala!

Bora utu,kuliko fedha zenye kudharirisha utu!

Umeitunza heshima yako;daima mashairi yako yatakua na thamani zaidi ya dahabu
 
Huyo mbona kashatumika sana na kina Ruge, sema labda hawajampa mchongo tu
 
Mpoto kitambo alikuwa kambi ya Samuel Sitta; kisha akahama kambi hadi kwa Membe... alivyoona namba hazisomi, akahamia kwa Lowassa!! So, issue ni mchongo... HAKUNA, narudia tena na tena, HAKUNA msanii wa kupewa mchongo wa kampenu halafu akakataa except wale ambao tayari wanafanya siasa za majukwaani! Hawa wote wanaojifanya sijui nini na nini ni kwamba ama hawakupata mchongo au offer waliiona ndogo!! Hivi kuna taasisi inayoongozwa kulalamikiwa na wasanii zaidi ya Clouds? What happens Clouds wanapotoa michongo kwa wasanii?
 
Yule anataman majukwa ya ccm ila manyimbo yake yanakinzana na utaratibu wa ccm

Mjomba alikuwa shujaa kwenye nyimbo mbili za mwanzo...tulimshaur vijana nenda kagombee ubunge kule kwenu ila sio kwa ccm maana utaangukia pua.......mafisiem yakamrubuni akaanza kutanga tanga km ayatooola zzk
 
Big up mingi kwake MJOMBA ila nalia na fid q sijui kampen ikiisha ataimba taarabu maana hip pop ni maisha halisi ye amehasi kwa kumpaka rangi donkey ili ageuke kuwa zebra
 
Big up mingi kwake MJOMBA ila nalia na fid q sijui kampen ikiisha ataimba taarabu maana hip pop ni maisha halisi ye amehasi kwa kumpaka rangi donkey ili ageuke kuwa zebra

Acha akili fupi, Fid ni fid hata iwe vipi unapomsikia kwenye wimbo hakuimbii maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…