Mrisho Ngasa fanya hivi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tunaofurahishwa na matokeo mazuri ya Yanga kwa kupitia juhudi zako uwanjani tuko wengi sana, wewe endelea kutupa raha uwanjani wana Yanga na sisi nduguzo tutasaidia kukulipitia deni lako linalokuzonga akili na kukuhamisha uwanjani (scratch our backs we will scratch your back too). Weka hewani namba yako ya simu na bank account ili wanachama na wapenzi wa Yanga wakuingizie pesa. Tuko nyuma yako, achana na akina Jerry Muro. Watu waliofurahishwa na mabao yako 2 dhidi ya mtibwa juzi ni wengi, hadi wengine walikufa kwa furaha ya kusherehekea ushindi dhidi ya Thobias Kifaru.
 
naomba kujuzwa huyu dogo ana deni gani linamzonga?
 
Ila yote tisa lakini nilikuwa sifurahishwi Ngassa kucheza dk7, alikuwa hajavurunda kiivo
 
Ukisikia fainali uzeeni ndio hiyo. Namshauri afungue saluni na shilole aendeleze career yake ya ususi
 
Natamani hizo hela mngewapa hata watoto yatima mngepata twawabu kwa Mungu. Ngassa ni mtu mzima na anawajibika kwa mambo yake ikiwamo madeni. Alichukua mkopo kwa shida zake na kulipa ni wajibu wake! Tusiwe na tabia ya kuendekeza kutowajibika.
 
Pole ngasa kwa kutokuona mbali. Na liwe fundisho kwa wachezaji wote vijana kuwa michezo yote kwa sasa ni kazi kama kazi nyingine. Mambo ya mapenzi na ushabiki wa timu fulani yamepitwa na wakati. Mara mnapopewa ushauri na hawa viongozi wa mpira changanyeni na akili zenu. Hawa viongozi hasa wa simba na yanga leo wapo kesho hawapo na wanapokuja wengine hawapendi kubeba mizigo iliyoachwa na watangulizi wao.
 
Natamani hizo hela mngewapa hata watoto yatima mngepata twawabu kwa Mungu. Ngassa ni mtu mzima na anawajibika kwa mambo yake ikiwamo madeni. Alichukua mkopo kwa shida zake na kulipa ni wajibu wake! Tusiwe na tabia ya kuendekeza kutowajibika.

Hatulipi deni la Ngassa bali tunalipia furaha. Kama kwa kumsaidia Ngassa kulipa deni lake kutasababisha aifungie Yanga mabao uwanjani basi tuko tayari kulipa deni maana tutakuwa tunaondokana na fedheha ya kufungwa na Mtibwa, polisi, mgambo, n.k. Hata wazungu ni hodari sana wa kulipia furaha, ndo maana club zinamwaga mapesa mengi kusajili wachezaji ghari duniani. Wakati sisi tunalipia deni la Ngassa acheze vizuri mpira wewe, Simba na Azam nendeni kalipieni mayatima ili mpate twawabu, tukimaliza deni tuta wa-join kwenye ibada hiyo.
 
naomba kujuzwa huyu dogo ana deni gani linamzonga?

Alichukuwa Simba sh. 30 mil ili kuichezea Simba badala yake akaikacha na kwenda kusaini Yanga ambayo inaichezea hadi sasa na kufunga mabao 2 dhidi ya Mtibwa juzi na kuifanya Yanga kuongoza ligi. hivyo akapigwa na riba ya sh. 10 milioni na kusababisha deni kuwa sh. 40 milioni. Sijui kashalipa kiasi gani hadi sasa. Kama kuna deni lingine anayelifahamu atatujuza hapa.
 

Hao mikia wamedhulumu hadi ya rambi rambi ya mafisango;wataweza wapi kuwachangia mayatima!
 
AHAHAHAHAAAAAA...SANGAAAAA..arghhh kumbe NGASAAAAAAAAAAA..pole dogo. ukuwe ujuwe....
 

Du! Kwa mitazamo hii waTz bado sana!!
 

Sasa Mkuu deni la Simba litaihusu nini benki? Wenzio wanaofahamu vizuri wanasema alikopa fedha benki ya crdb na Yanga akawa mdhamini wake kwa makubaliano kwamba mshahara utapitia benki ili wakate hela yao! Sasa uongozi uliopita haukutekeleza hilo kwa mwaka mzima, ndo benki imewafuatilia Yanga juzi nao ndo wakaanza kuupitisha mshahara huko! Haya ni kwa mujibu Wa Muro wakati anahojiwa na Mawingu FM!
 
cOmpLicateD, hata hivyo kama Ngassa ana uwezo wa kutupa raha wana Yanga tusaidie tu, maana hata OKWI mganda anahomola mapesa ya watanzania na bado anasumbua kinoma, pamoja na hayo bado OKWI yumo tu kwenye first eleven ya timu zetu kutokana na uwezo wake miguuni, sembuse huyu mtanzania mwenzetu aliyeiwezesha yanga kuongoza ligi japo inaweza kuwa ni kwa muda. Mchezaji mwenye psychological problems na frustrations hawezi kucheza mpira kwa kiwango chake
 

Aise kumbe issue iko hivi! Sasa huyu dogo Mrisho analialia nini kwenye media? Mbona huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa mwajiriwa kukopa kwa udhamini wa mwajiri wake. Kamwe jukumu la msingi la kulipa deni halijapata kuwa la mdhamini.Unless angetwambia Yanga FC haimlipi mshahara wake. Lakini mshahara analipwa na mkopo alichukua kwa matumizi yake binafsi still anarudi kulia kwa wanayanga? Come on Ngassa,,,embu wajibika bwana.

Halafu hawa wachezaji wetu ni wakati sasa waachwe wavune wapandacho. Kila kitu wanajivika ujuha tu hata washauriwe vipi. Mikataba yao ya kazi tu wanajisainia hovyo wakati siku hizi mawakili wako hadi vichochoroni na reasonable consultation fees. Kama hakufahamu taratibu za mikopo angetafuta wataalamu wa kibenki na sheria kabla si kulalamika hovyo.

Aachwe awe mfano kwa wengine huyu ama la Yanga mkiamua kumlipia hakikisheni mnaingia nae makubaliano fulani hata ikibidi kusaini mkataba bure wa kuichezea club pindi mkataba wake wa sasa ukimalizika.
 

Duh mengine ya kujitakia aisee, Kwa hiyo yeye mwaka mzima hajakatwa ameuchuna tu!!
 
Ina maana kwenye akaunti yake Milioni hizo hazifiki alipe? :/
 
Ngassa kuna kitu anazugia na mtakisikia hivi karibuni
 
ishakua tabu yaani kutupia tugoli tuwili tu...hadi anapata coverage kwa media, na huyu msemaji wa Yanga ana akili kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…