Simba ataweza kugombea namba ba shiza kichuya? Labda aende mbao fcAje kuifunga Simba
Hahah teh teh teh acha nipite nikachek mazoezi "we mbayaaaa!!!Kwanza mapungufu yake yameanza tu kuonekana kuanzia katika hilo jina lake la katikati. Haitwi Alfan bali tunaomjua tokea Kitangiri na Mecco Mkoani Mwanza tunamjua kuwa jina lake la katikati ni Khalfan sasa sijui hilo la Alfan alibatiziwa upya wapi tena na huu ndiyo ULIMBUKENI wa Waafrika baadhi kutaka kujifananisha na Wazungu.
Nirudi katika suala la msingi juu ya kilicho mezani kumuhusu huyu Mchezaji. Kuna mahala humu humu JF niliwahi kuandika post fulani kumuhusu Mrisho Khalfan Ngassa alipopata tu hilo deal la kwenda katika hiyo Klabu huko Afrika ya Kusini lakini nikaonekana namchukia kwakuwa tu Mimi ni " Mnyama Mnyamani ".
Sishangai leo kusikia kuwa Mchezaji Mrisho Khalfan Ngassa yamemfika yaliyomfika huko alipo. Matatizo makuu yanayomkabili Ngassa japo yapo mengi ila haya yafuatayo ndiyo makubwa:
Asubuhi njema.
- Umri. Ngassa hana umri huo ambao wengi tunadhani anao na nina uhakika kuwa Ngassa sasa ana miaka kati ya 31 au 33 ila wengi tunadhani ana miaka 24 au 27. Wachezaji wengi wa Kiafrika wanaodanganya umri wakiumia tu kidogo Jeraha huchelewa kupona.
- Utoto. Ngassa ameshindwa kujitambua kuwa Yanga, Azam na Simba ambazo alizichezea siyo Free State na Klabu zingine za South Africa au huko Ulaya ambazo kimsingi zina maadili na nidhamu ya Soka tofauti na huku kwetu ambako kumejaa tu uhuni uhuni.
- Starehe. Ngassa anapenda sana kula " bata " yaani kustarehe na kwa mujibu wa Mtanzania mwenzie aliyepo huko huko South Africa anasema kuwa Ngassa amewekeza mno katika Starehe. Kwa tunaomjua Ngassa tokea akiwa hapa Dar ilikuwa ni nadra sana kila Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi kumkosa Ngassa katika kumbi mbalimbali ila uwanja wake wa nyumbani ulikuwa ni Mango Garden. Na ni huyu huyu Ngassa ndiye aliyemuharibu na kutaka kumpoteza Kiungo wa Simba wa sasa anayefanya vizuri Jonas Gerald Mkude kwa kumuingiza katika ulevi wa kupindukia hadi kupelekea siku moja Mkude alizima kabisa kwa " kupombeka " hapo Mango na ikabidi akina Singano " Messi " waitwe kumbeba huku akiwa " chakari " na hajitambui.
- Umalaya. Ngassa anaendekeza mno matumizi mabaya na ya kupindukia ya PAPUCHI. Hiki kitoto kimetoka tu West Ham kikiwa kimeambiwa kuwa kije kifanye mazoezi tena ambayo alikuwa ameshapangiwa kabisa yeye alipotua tu Bongo land haraka bila kuchelewa kakimbilia kukidaka Kidemu kimoja Kawe mwisho eneo la Maringo na kama hiyo haitoshi tena akaanzisha uhusiano na Jimama moja mitaa hiyo hiyo ya Mango Garden sasa hii tisa na kumi wakati Ngassa akijua kabisa kuwa anatarajia kumuoa huyo Mkewe aliyenae sasa akaanzisha mahusiano ya " Kingono " na Msanii wa Taarab kutoka Mkoani Mara ambaye hupenda kujiita QUEEN OF THE BEST MELODY na kama kuna Mwanamke anayemfanya Ngassa kila mara akili zake ziwe Dar ni huyu Mwanadada kwani Ngassa atafurukuta kwa wote ila kwa huyu Dada amekufa na kaoza.
- Matumizi ya Pombe za Makaratasi. Ngassa na Wachezaji karibia 90% hapa Tanzania ni Watumiaji wa kutukuka wa Pombe ya Makaratasi a.k.a Urithi wa Bob Marley japo mpaka sasa hajamfikia Gwiji wa hiyo kitu Haruna Moshi " Boban " hivyo basi huko alipo Ngassa anakosa uhuru wa kukitumia hicho Kilevi kutokana na nidhamu ya Soka waliyonayo wenzetu. Pombe ya Makaratasi huwapa sana " mzuka " wachezaji wa Bongo japo wengi wao huwaathiri hadi kupelekea kuwa na maamuzi ya kustaajabisha kama Beki wetu wa kutumainiwa wa Taifa Stars ambaye juzi tu ameitwa Taifa Stars lakini akagoma kwenda na huyu mchezaji nadhani Kicheo kwa matumizi ya Pombe ya Makaratasi anaweza akawa ni Naibu kwa Haruna Moshi " Boban ".