Mrisho Ngassa atua rasmi Free State Afrika Kusini

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
View attachment 251238

Club ya Free State inayoshikilia nafasi ya tisa ktk ligi ya nchini Afrika Kusini tayari imemsajili Mrisho Khalfani Ngassa kwa mkataba wa miaka minne kkt kuitumikia timu hiyo.

Akiongea baada ya kukabidhiwa jezi ya team hiyo Mrisho Ngassa amesema "Sasa nimejiandaa kwa maisha mapya,baada ya kucheza ligi ya nyumbani Tanzania kwa muda mrefu.Nitajitahidi kuitumikia timu yangu ili kutangaza jina la Tanzania nje ya mipaka ya nchi,na ili timu za Afrika Kusini zifikirie tena kusajili wachezaji kutoka Tanzania na kukuza soka la nyumbani"

Naye kocha wa FS Mmalawi Kannah Phiri amesema, alimfahamu Ngassa kwa muda mrefu na kuvutiwa na soka lake zuri,imekuwa ni furaha kwake kukutana na kufanya kazi na kijana huyo ktk Club ya Free State
 
Kila la kheri kijana,hili ulipaswa ulipaswa ulifanye kitambo sana wakati ule una miaka 20,badala ya kuwa na mawazo ya kucheza ulaya,wewe ukajitajidi kuwaonyesha watu jinsi gani unaipenda Yanga,hayo ni mambo ya kizamani mno...hujachelewa kijana kaza buti SA iwe njia ya kukufikisha PSG..
 
Ni baada Yanga kumshusha thamani.Sasa awa lulu bondeni.
Gari atakayopewa ni mpya kabisa BMW made ya S.AFRICA.
Kila la kheri NGASSA.

My take:
Yanga wamuuze na Msuva,otherwise nae ataondoka free mwezi jan.
 

Attachments

  • 1.jpg
    25.5 KB · Views: 1,664
kuhusu msuva km watagoma kumuuza inabidi anunue mkataba wake......vinginevyo itakula kwake
 
Mmmh !! wasije wakasema kaenda kuchukuwa ajira za wa Sauzi !?! Hao wasauzi hawaminiki tena......Hongera Mringassa!!
 
Kila la kheri Ngassa.Nahakika sasa utafanikiwa ngono za kibongo zilikua zinakuharibia soka lako.
 
wapi hizo details za stahiki zake mkuu?
 
Mkataba wa muda mrefu hauna shida yoyote maana klabu yoyote itayomuhitaji italazimika kutoa ngawira hapo...

Na pia huenda wamemuona Ngassa ni lulu yenye thamani ya kuwatumikia kwa muda mrefu...

kumbe wamempa mkataba wa muda mrefu hivi!!! Hii imekaaje kisoka wakuu

cc Makoye Matale, mkolaj, Watu8 n.k
 
Last edited by a moderator:
Mkataba wa muda mrefu hauna shida yoyote maana klabu yoyote itayomuhitaji italazimika kutoa ngawira hapo...

Na pia huenda wamemuona Ngassa ni lulu yenye thamani ya kuwatumikia kwa muda mrefu...

So pia kuwa strategy ya kumbana mchezaji asiwakimbie??

Nashangaa hapa kwetu naonaga wanapewa miaka 2 au mwaka tu basi, ndo maana nikashangaa hiyo miaka 4 ya Ngassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…