msaaada kuhusu picha ya nyerere

Kiwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
2,102
Reaction score
907
wakuu naomba msaada. nimepita katika kijiwe kimoja nikasikia vijana wanabishana kuhusu mambo ya siasa. kimoja kati ya walichokuwa wanabishana ni kwamba hayati mwalimu nyerere alikuwa havai nguo za chama chake CCM.
waliponiona waliomba maoni yangu kuhusu hilo.kiukweli binafsi katika kumbukumbu yangu sijawahi kuona.nimejaribu kutafuta nimekosa.
mwenye nayo ebu naomba atuwekee hapa ili hawa vijana wamalize ubishi wao.
asante.
 

Mkuu hata mimi sijawahi kuona akiwa amevaa jezi ya CCM. Lakini pia kumbuka ya kwamba mambo ya jezi yalianza baada ya kuingia kwa vyama vingi hapa nchi kwa sasa yameshamiri sana. Sijui kama ni chanzo cha mapato kwa vyama ama la. Huenda angekuwepo hadi sasa angekuwa anavaa.

 
Ni kweli yameanza baada ya vyama vingi, lakini hata alipozunguka nchini kumnadi Mkapa mwaka 1995, pamoja na kwamba kulikuwa na fulana na kofia za Mkapa, hakuzitumia. Hata hivyo, ukipata picha ya mkutano mkuu wa CCM 1987 Kizota, mwalimu alivaa shati la kitenge maalum kwa mkutano huo sawa na wajumbe wengine wote wa mkutano.
 
nyerere alikuwa ni mtaifa kwanza, wengine wanalinda maslahi ya chama kwanza thn utaifa baadae.
 
Labda tujiulize swali moja, CCM wameanza lini kutumia jezi zao ?
 

kama hajawahi kuvaa tujiulize ni kwanini mkuu.je aliona sare haina maana yeyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…