Msaaada wa mawazo ndungu zangu.

kaaa

Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
35
Reaction score
4
Nimepigiwa simu na watu wa recruitment service wapo mwenge karibu na sheli moja vipi.Eti wameniambia nipeleke cv zangu jumatatu.Najiuliza wameipata wapi namba yangu?wanataka kuniuliza nini?maana mimi sijawahi hata kuomba kazi kwao?hawajaniambia nimeomba post gani na katika kampuni gani?Sio matapeli kweli?Msaada wajemeniπŸ™‚
 
Mhh...,we nenda kawasikilize halafu waulize maswali yako yote kwani waswahili wanasema kubali wito....Mungu akutangulia .
 
Angalia ndugu yangu icjekuta ni wale wachuna ngozi wameingia kwene system nyingine ya udanganyifu wakakutoa roho bure. Kwani ukifikiria kupata kaz kulivyo kugumu halafu unaitiwa kaz tu from no where na wewe hujaomba; ni hatari.
 
Nashukuru wakubwa kwa ushauri wenuπŸ™‚ Nitazingitatie vyote.
 
Ujipange lazima ubebe silaha
 
Freemason hao...ha ha ha ha ha ha ha
 

We nenda na hiyo CV ila wakikwambia uwape pesa hata 100 kataa.

Lazaid kawaulize maswali utajua km ni matapeli au siyo.
BY DA WAY WAKIKUAMBIA MKAKUTANE VICHOCHORONI KATAA.
ALL THE BEST.
 
Wapigie uwaulize. kama haupo comfortable usiendi. Ila kumbuka, kama ulitoa CV kwa recruitment service nyingine, huwa wanashare details zako, unless specified otherwise.
 
Nashukuru sana Ndugu zangu, nimepata mawazo mazuri sana ambayo sikuyategemea. Idumu jamii forums!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ulipowauliza walisemaje? Kwa nini unaenda kama hukuomba kazi. Wanaenda kukutumbukiza kwenye concentrated sulphuric acid, hutabakia hata mfupa, shauri yako we nenda uone.
 
Acha njaa ya kazi wewe hao matapeli unayajua leo na ukienda huko watakuambia uwape pesa sasa kuwa makini sana. Kataa wala usiende wala nini wengine wanatumia dawa sana kuwaibia watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…