Msaaada wenu kwa mwenye uelewa wa jambo hili

Fast Forward

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
551
Reaction score
709
Habari za weekend wakuu, poleni na majukumu.
Naomba nitangulize tahadhari kwa asiyekuwa na wazo/mchango juu ya hili asicomment chochote au kutoa ushauri wa kubeza maana wengi hufikiria kila kitu ni masihara na porojo za vijiweni

Kuna mwanamke anasumbuliwa sana na suala la kutokula japokuwa ni mjamzito wa miezi 3 na wiki 1 ila hali ilipofikia sasa anaweza kukaa ata siku mbili hajala hii hali kwa kweli hata mimi imenishangaza kwa kawaida najua anaweza asile kutwa nzima lakini huyu ni siku mbili sasa hii imenishangaza kama kuna anayejua hili anifahamishe kwa muda huu japokuwa kesho anampango wa kwenda hospitali
Kwa mwanamke ambaye aliwahi kukumbana na hali hii kipindi cha ujauzito wake anifahamishe ata kwa pm tumsaidie huyu mwanamke mwenzenu maanà hali unapoendea sio nzuri na uzazi huu wa siku hizi mtu akijifungua salama ni jambo la kushukuru sana
 
Suluhisho ni kumuwahisha hospitali mapema iwezekanavyo\
Hilo tatizo si geni...tiba yake ipo endapo utawahi mapema zaid kwa matabibu
 
Mimba huwa zinakuja kwa staili tofauti sana, mwingine anaweza kupenda jmaji tu na chakula akawa hali aisee....., pia kama bado ni changa chini ya 12 month huwa zinasumbua sana. na mara nyingi vitu kama hivi huwa havichukui mda mrefu vinakwisha tu, usiogope sana hawezi kukaa mda mrefu bila kula lazima atakula tu.

Mimba ni ugonnjwa mzuri ambao staili zake ni tofauti na hazieleweki. ukiona hali inazidi anapita hata siku 4 mpaka 5 au wiki bila kula, tafadhali mpeleke hospitali, na kama hajaanza clinic aanze maramoja.
 
​kuwa mpole kiongozi hata wa kwangu ilikuwa hivyohivyo ila baada ya miezi mi3 kupita ataanza kula hadi utakasirika kudhani anafuja
 
​kuwa mpole kiongozi hata wa kwangu ilikuwa hivyohivyo ila baada ya miezi mi3 kupita ataanza kula hadi utakasirika kudhani anafuja

Sawa mkuu ila huyu tayari ameshafikisha miezi mitatu na hali hii ndio imezidi kuwa mbaya
 
12 weeks


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…