Msaad unahitajika

mr.MDAU

Member
Joined
Apr 14, 2013
Posts
36
Reaction score
3
Kuna jamaa kanitembelea ni rafiki yangu anasumbuliwa na fizi za meno kutoa damu anapopiga mswaki kwa anaejua namna ya kumsaidia. Plz! Anadai eti kuuma haziumi ni meno tu huwa yanauma anapoweka vitu vyenye sukari Mdomon
 
Hivi wewe na huyo jamaa yako hamjui hospitali mahali zilipo?
 
Mwambie rafiki yako aende kwa daktari wa meno akasafishe meno kwanza.

Baada hapo afatishe maelekezo ya kupiga mswaki vizuri kutoka kwa huyo daktari na atapona tatizo lake.

Kwa sasa anaweza kusukutua kwa kutumia hydrogen peroxide. Ni muhimu kwenda kwa daktari wa meno kusafisha hayo meno na baada hapo apige mswaki mara mbili kwa siku asubuhi na usiku kabla kwenda kulala na pia lazima ku-floss meno yake kila baada ya kula.

Kusukutua kwa maji ya vuguvugu ya chumvi yatasaidia kupunguza uvimbe wa fizi lakini lazima akasafishe meno kwa dentist.
 
huo ugonjwa unaitwa kiseyeye unatibiwa kwa kuramba ndimu nilijifunza tibayake nilipokuwa darasa 3 somo la sayansi kimu, chezea enzi za MWALIM wewe
 
Meno hayaumi akila na kunywa vitu vya baridi?
Muambie aende kwa dentist. Kama msaada mnaotaka sio wa hospitali, hapa huduma ya uganga na uaguzi tumeifunga kwa muda.
 

nlikupata mkuu! Jamaa anapata doz kwa sasa! Mlemle!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…