Msaada AC ya Gari langu Runx

Msaada AC ya Gari langu Runx

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu Habari.

Kuna gari hapa, Toyota Runx inasumbua kidogo AC. Hafu ndio mchezo wake kila baada ya miezi kadhaa.

Mara ya kwanza nilipeleka kwa fundi akasema hakuna leakage. Akajaza Gesi. Hapo AC utaanza kuiona ona kwa muda wa miezi kadhaa.

Ila muda ukienda inapungua nguvu. Unaanza kuweka Maximum. Upepo unatoka kwa nguvu tu ila hauna ubaridi.

Nikijaza tena gesi inakua afadhali ata ukiweka Low bado unasikia ubaridi. Ila muda ukienda (miezi minne hivi) tatizo linarudi tena.

Kwa ili joto la Dar ile hamu ya gari haipo sana. Esp mkiwa foreni na mchana.

Msaada hapo. Mafundi zaidi ya wawili wanasema leakage hamna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshapata tatizo kama hilo....hapo ishu ni leakage....fundi anayesema hakuna leakage huyo hajui kazi yake....hususani ukute gesi inavuja ndani kwenye evaporator...ni ngumu kwa fundi wa kawaida ambaye yupo after money kugundua hili.

Bahati yako mbaya upo mbali...ungekwa Arusha kuna jamaa yupo vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana boss. Coolant ipo poa. Ata Gauge ya Temp ipo vizuri tu.

Tatizo ni joto tu la ndani. Yaani joto ova umejifungia kwenye hotpot. Ukifungua madirisha hadi chini ndio kuna unafuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu feni zinazunguka sawa sawa? Mm yangu ilipata shida ya fan mortal iliungua gari ikawa inachemka Kwahiyo automatically ac ikawa inaingiza joto hatari niliponnua fan ac ikapiga mzigo burudani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshapata tatizo kama hilo....hapo ishu ni leakage....fundi anayesema hakuna leakage huyo hajui kazi yake....hususani ukute gesi inavuja ndani kwenye evaporator...ni ngumu kwa fundi wa kawaida ambaye yupo after money kugundua hili...
Bahati yako mbaya upo mbali...ungekwa Arusha kuna jamaa yupo vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitaka kushauri hivi, ile pipe inayoingiza gas kwenye evaporator, Ile connector inaweza kuvujisha gas na kama fundi ana haraka anaweza asijue, inahitaji utulivu kidogo...
 
Nimeshapata tatizo kama hilo....hapo ishu ni leakage....fundi anayesema hakuna leakage huyo hajui kazi yake....hususani ukute gesi inavuja ndani kwenye evaporator...ni ngumu kwa fundi wa kawaida ambaye yupo after money kugundua hili...
Bahati yako mbaya upo mbali...ungekwa Arusha kuna jamaa yupo vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi nipo AR na ninashida kama ya jamaa hapo juu (NB: Gari yangu ni RV4),. Nisaidie mkuu wangu.
 
Kwa wapi mkuu? Au ni fundi wa hapo ndani gereji ni kwa pale nyuma wanapouza madafu?
Ndiyo... opposite na gorofa la Manjis.

Mtafute jamaa mwenye hiyo namba...si manyoka wake....nilikuta anaziba leakage kwenye gari za maana sehemu amabzo hautadhania
 
Yaani hapo nasweat jasho hatari hakuna ata punje ya ubaridi
1550925406602.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishika zile pipes za coolant kwenye boneti lazima moja iwe ya moto moja ya baridi fanya kuzigusa ukiwa umewasha A. C then uje utupe mrejesho
 
Back
Top Bottom