kuna jirani yangu ameniomba ushauri kuwa yapata mwaka mmoja sasa ameoa ila hawajajariwa kupata mtoto,ndio juzi akaenda hospital akafanyiwa sperm analyiss,ikaonekana total sperm count yake ni milioni 15!na akaambiwa kuwa ili kuwa na uwezo wa kupatisha mimba ni lazima zisipungue milioni 20.mtu wa maabara ndiye alimpa majibu hayo,kwani dr,aliyemwambia akafanye vipimo hivyo amesafiri,Ndiyo nikamwambia ngoja nikawaulize wataalaam wa JF,tunaweza kupata wapi pa kuanzia.Labda kuna vyakula anatakiwa awe anakula sana au atumie dawa gani.