Kitumburee
Senior Member
- Jan 31, 2012
- 142
- 88
Habari zenu wana jamvi, naomba msaada wa kisheria.
Nilinunua eneo Mabwe pande, eneo linaitwa Kinondo kijiji cha Utulivu mwaka 2017. Eneo hili lina documents za serikali ya mtaa ila halina hati. Tangu muda huo nimekuwa nikilima mihogo na nimeweka alama za mipaka katika eneo langu.
Cha kushangaza nilienda wiki mbili zilizopita nikakuta mtu anajenga hapo akidai kuwa ameuziwa eneo hilo na ana hadi documents za serikali ya mtaa. Nikamshtaki polisi, nikaenda kwa Mwenyekiti wa Mtaa kutoa taarifa na Ofisi ya Mtendaji pia, Mtendaji akaandika katika hilo jengo kuwa ujenzi usimamishwe. Cha kushangaza yale maandishi yamefutwa na ujenzi unaendelea.
Muuzaji ndiyo yule yule aliyeniuzia mimi na kwa sasa amekimbia. Kamati ya usulihishi ya kijiji haina msaada wowote kwangu kwa sababu hiyo hiyo kamati ndio ilihusika katika hayo mauzo ya huyu jamaa.
Naombeni ushauri nifanye nini?
Eneo hilo watu wengi sana wamedhulumiwa viwanja vyao na jamaa mmoja anaitwa Imma ambae yumo katika hii kamati ya usuluhishi. Majirani zangu wanadai waliogopa kunishtua walivyoona eneo linauzwa kwa kumuogopa huyo Imma kwa sababu anawatishia maisha yao.
Kamati hii ya usuluhishi haina msaada kwa kigezo kwamba aliyejenga ndio atapewa kiwanja haijalishi ameuziwa lini.
Naombeni ushauri nifanye nini.