Msaada: Ana mimba au?

umurumaithaa

Member
Joined
May 9, 2015
Posts
70
Reaction score
8
Habari zenu ndugu zanguni, natumai ni wazima,

Nina ndugu yangu alikua na Malaria lakini kabla ya kwenda kucheki alikua anajiskia vibaya (kichefuchefu kizunguzungu) tukahofia isije ikawa mimba. Siku tuliyoenda kucheki Malaria, tulinunua na kifaa cha mimba.

Malaria kakutwa nayo 3, mimba hakuwa nayo na siku hiyo hiyo alipata siku zake japo alichelewa (kavuta sana toka tarehe 20 mpaka 25 ndo kapata).

Sasa shida ipo hapa; toka amalize dose ya Malaria bado anasikia kichefuchefu, kula hawezi na sometimes kizunguzungu, moyo kwenda mbio, hataki kusikia harufu ya mafuta ya kunukia na jana maziwa yake yalikua yanatoa maziwa na kumuuma.

Naombeni msaaada, samahani kwa maelezo marefu.

Shukrani
 
Cha muhimu kama hayo yanaendelea ni kwenda kuchekiwa na Dr kiundani kama kufanyiwa vipimo vya damu, mkojo etc

Dawa pia inaweza kuwa sababu ya yeye kuwa hivyo.

Au akae mwezi aone kama itapungua na zikija siku zake zingine za hedhi basi akaendelea kuwa hivyo au ikazidi basi ni kukimbilia hospitaki sababu kunaweza kukawa na kitu kinachofanya awe hivyo.

Kama unazania mimba basi hata kwa damu itaonyesha kama anayo au hana mimba.

Kama mna wasiwasi sana ni kwenda hospitali haraka.
 

Asante sana kwa ushauri
 


Huwezi kupata Amenorrhea kama kuna mimba.


Azungumze na daktari vyema huenda kuna tatizo jingine.


Allergy may be!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…