Habari waungwana!
Nina kijana wangu wa kiume nataka nimpeleke secondary ya bweni. Ombi langu ni kwa ambaye anaifahamu shule mojawapo ya bweni inayofundisha vizuri au ameisikia kutoka kwa jamaa wa karibu.
Nahitaji iwe mkoa wa IRINGA au SONGEA. Na kama utakuwa na mawasiliano ya shule husika utakuwa umenisaidia sana. Natanguliza shukrani.