Mkuu
Travellerman wakati wanakushauri hayo mengine, naomba uanze tumia viazi mviringo (wengine huita viazi mbatata),
Chukua kiazi kimoja chenye ukubwa wa wastani, osha vyema, menya kisha kwangua (tumia kwangulio la karoti),
Kisha fanya kama unamasejia uso, rudia hivyo mpaka uone yale maji maji ya kiazi yamekwisha yamebaki yale makapi tu..!!
Acha usoni kwa masaa kuanzia mawili na kuendelea, kisha nawa uso wako vyema, uache bila kupaka chochote kwanza, hii itafaa zaidi ikiwa inafanyika usiku..!!
Ukiamka asubuhi, utaona tofauti, rudia zoezi hili mara kwa mara, utaona matokeo ya haraka zaidi, kila la kheri..!!