Msaada: Anayejua kuhusu Karaga Mti (macadamia nuts)

Msaada: Anayejua kuhusu Karaga Mti (macadamia nuts)

Matindi94

Member
Joined
Oct 12, 2016
Posts
47
Reaction score
50
Habar za kazi wana JF naomba kujua kuhusu kilimo cha hili zao

Je, mbegu zake zinaweza kupatikana wapi?

Je, soko lake lipoje na linawez kustaw maeneo ya baridi kama vile Njombe na Iringa?

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Mimi nazipenda sana nilibahatika miche miwili nimepanda nje kwangu Mungu akijalia uzima ndakuja kuzila.
 
Macadamia nuts zinastawi zaidi kwenye maeneo yenye muiinuko, mvua ya kutosha na kiwango kidogo cha joto. Wataalamu wanasema mikoa ambayo zao la migomba, kahawa na chai linastawi vizuri basi Macadamia nuts pia zinastawi.
Mikoa ambayo zao hili linastawi zaidi ni Njombe, Kilimanjaro, Arusha, Tanga (wilaya ya Lushoto), Uluguru mountains, Mbeya.
Ingawa mikoa mingine pia zao hili limeonyesha matokeo mazuri.

Mavuno ni baada ya miaka 4-5 na mti huzaa mara 3 kwa mwaka.

Kenya pia wanalima zao hili lakini wanapendelea zaidi macadamia nuts za Tanzania sababu zinalimwa bila kutumia kemikali,hii inasaidia kuongeza ubora wa nuts za Tanzania. Wafanya biashara wengi wa Tanzania hupendelea kuuza nuts zilizokaushwa tayari au mafuta ya nuts

1kg ya nuts zilizokaushwa ni sh elfu 20
 
20210123_143441.jpg
 
Heka moja inaingia miche mingap
kwa space ya 4.5*4.5m itahitajika miche 245 kwa eka moja.

Kulingana na swali lako umeuliza HEKA moja,ambapo 1 hekta=2.5eka
2.5×245 = 612.5
Itahitajika miche 613 kwa heka moja

Kama nitakuwa nimekosea kwenye vipimo,naomba kusahihishwa
Heka moja inaingia miche mingap
 
Yaani hivi tumevila sana utotoni,wenyewe tulikuwa tunaviita vinazi.issue kuvunja ganda lake gumu balaa
 
Back
Top Bottom