Macadamia nuts zinastawi zaidi kwenye maeneo yenye muiinuko, mvua ya kutosha na kiwango kidogo cha joto. Wataalamu wanasema mikoa ambayo zao la migomba, kahawa na chai linastawi vizuri basi Macadamia nuts pia zinastawi.
Mikoa ambayo zao hili linastawi zaidi ni Njombe, Kilimanjaro, Arusha, Tanga (wilaya ya Lushoto), Uluguru mountains, Mbeya.
Ingawa mikoa mingine pia zao hili limeonyesha matokeo mazuri.
Mavuno ni baada ya miaka 4-5 na mti huzaa mara 3 kwa mwaka.
Kenya pia wanalima zao hili lakini wanapendelea zaidi macadamia nuts za Tanzania sababu zinalimwa bila kutumia kemikali,hii inasaidia kuongeza ubora wa nuts za Tanzania. Wafanya biashara wengi wa Tanzania hupendelea kuuza nuts zilizokaushwa tayari au mafuta ya nuts
1kg ya nuts zilizokaushwa ni sh elfu 20