Msaada: Anko wangu amechanganyikiwa

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2019
Posts
228
Reaction score
210
Ni mjomba wangu wa nne yaani baada ya mama anafuata anko Gervas Tibaijuka then anakuja yeye.

Tangu afukuzwe kazi mjomba wangu amekuwa ni mtu wa kunywa pombe na kula wanawake tu. Imefikia hatua hadi anashindwa hata kulala kwake.

Nyumbani kwake anaacha tumizi la Tsh. 100,000 tu kwa siku. Just imagine familia ya watu wanne unaachaje tumizi la laki moja tu? Unataka familia ife njaa?

Mbaya zaidi mtoto wake wa kwanza (Grace) amemrudisha kutoka Massachusetts, Marekani eti amekosa ada. Na wakati anaonga mahawala zake hadi Kluger!

Juzi ndio ametuacha hoi wana ukoo eti ameamua kumpeleka Steven, mtoto wake wa pili na wa mwisho shule. Tukamuuliza utampeleka wapi? Eti akasema DIA! ile shule ya Dar Es salaam International Academy.

Masikini mjomba! Kweli maisha ni kupanda na kushuka. Amefikia hatua ya kumpeleka mtoto shule ya elimu bure kiasi hicho! Eti mtoto Kindergarten nyie mnaita chekechea wanalipa Tsh. Milioni 27 tu kwa mwaka. This is nervous jamani.

Anakoelekea anaenda kudhalilisha ukoo wetu. Sitakubali cousin wangu asome shule za ajabu kama hizo. Japokuwa sina ajira kwa sasa. Nitajitahidi mwakani nimlipie ada asomee kama sio US basi UK.

Mnapokuwa kwenye sala naomba mumkumbuke mjomba wangu ili aache starehe na kutelekeza familia yake kiasi hiki.

Jambo Tanzania.
 
Ni ngumu sana kumuelewa mtu aliyeJoined JF Oct 2019, bado upo under probation mdau, Hongera sasa umetimiza mwezi mmoja lakini bado una mengi yakujifunza !
 
Ngoja waje uone utakavo nyooshwa na vile unaitwa Rutashobolwa.....
 
Nmeishia hapo uliposema matumizi ya laki1 kwa siku ni madogo kwa watu wanne siendelei kusoma huu ujinga maana kuna watu wanabajeti ya 2000 kwa siku na maisha yanaenda
Usichukulie kila kitu serious humu,hasa kwa watu dizaini ya mtoa mada.
Humu ni kama kijiweni,sehem ya kupiga soga na kupunguza stress!
Mleta mada anaishi kwa mume wa Dada yake na ni wa mwisho kulala na wa kwanza kuamka maana yake analala 'sebleni'.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha nicheke tu maana nikitukana nitaishia kula ban kwa ajili ya mjinga mmoja
 
Hahahaha tumizi la laki moja familia ya watu 4 kwa siku! Ama kweli itakufa njaa
 


Iwee, nshomile,🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…