Msaada: "Baba Mkwe ananinyatia!"

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Monday, August 09, 2010 10:53 AM
MSICHANA mmoja jina kapuni [25] mkazi wa Banana jijini Dar es Salaam, amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuchoshwa na vitabia anavyoviita vichafu anavyofanyiwa na baba mkwe wake hali inayomfanya kutamani kuhama ndani ya nyumba hiyo. Msichana huyo alidai kuwa, baba mkwe wake amekuwa na tabia anazodai ni za utovu wa nidhamu ambazo hazistahili kufanyiwa ikiwa kama mkwe wake na anakwenda kinyume na tamaduni za kitanzania.

Msichana huyo mrembo mfanyakazi wa benki ya NMB amedai anakwazwa na mkwe wake kwa kuonyesha dalili za kumtamani hali inayomfanya akose raha na kuogopa kumwambia mumewe wake, kwa kuwa angeweza kuhatarisha ndoa yake ambayo ni changa.

Alidai kuwa mume wake ambaye pia ni mfanyakazi wa benki hiyo lakini walikuwa katika matawi tofauti ya utumishi, walioana mwishoni mwa mwaka jana.

Alidai kuwa mkwe wake huyo, ambaye ni mwalimu mstaafu alikuja kuishi nyumbani kwake hapo tokea Machi mwaka huu, akitokea mkoani Kilimanjaro na amekuwa akimfanyia vituko vya hapa na pale hali inayomfanya akose raha na nyumba yake.

Alidai kuwa baba huyo mwanzoni kabisa alikuwa akiona mwanae ametoka na kuaga,baba huyo amekuwa akiingia chumbani kwake bila hodi hali iliyoimfaya amshangae na akifanya hivyo hujitetea na kumwambia kuwa amuandalie aidha chakula ama kumuuliza kitu chochote huku yeye akiona yuko sahihi.

Alidai hali hiyo ilijirudia mara mbili hali iliyomfanya akaombe ushauri kwa nduguze huku bila kumdokeza mumewe tabia anazofanya baba yake ya kuingia chumbani kwao.

Alidai baba huyo alikuwa akimfanyia vituko vya aina mara aombe wale chakula kwa pamoja, mara nyingine amsifie kuwa ni mrembo sana, na kupigia simu mara kwa mara akiwa kazini mara nyingine akimuhimiza awahi kurudi kwa kuwa amemkumbuka.

Alidai kuna siku baba huyo alimshika sehemu zake za makalio alijisikiavibaya na kuingia ndani kwenda kumwaga machozi kwa uchungu kutokana na hali hiyo.

" Hofu yangu siku moja huenda atanibaka, simuamini sijui nimwambie mume wangu? alijiuliza

Hivyo dada huyu alikuwa anajaribu kuomba ushauri kwa wasomaji wa mtandao huu
 
mmh pole sana
amwambie mume wake ajue
km mume ni mwelewa ataelewa tu cz babake si malaika so atajua tu babake pia ni kma walewale
-usikubali kumezea hali hii kwa sababu meumeo akijua atashndwa kuelewa araka araka na uyo ni mkweo si kama unaweza kumpotezea km mtu baki so cha kufanya mwambie mumeo mlikablil swala ili
-pole sana.also mtimizien araka mahitaj yake araka ili apate kusepa
 
aisee wachaga nouma, niliwahi kusikia kuwa ukimpeleka mkeo ukweni (kwa wachaga tu) baba mkwe lazima arambe kumbe ni kweli!
 
Kwa kweli hilo ni bahati mbaya. Nashauri umwambie mumeo lakini kwa kuhakikisha kuwa lazima kuwepo na uwezekano wa uthibitisho mf. kama aliwahi kukutumia sms. Kama kuna siku unadhani atafanya kituko, awepo mumeo na huku yeye bila kufahamu kwamba yupo ili mumeo amwone laivu.

Umakini unahitajika kwani baba huyo asiweze kutumia mwanya wowote kukugeuzi kibao kwamba wewe ndiwe unayemtaka baba mkwe. Hivyo mumeo asije akaungana na baba yake.
 
Unakaa kwenu au unakaa kwa baba mkwe! Kijana kama ameoa na anakaa kwa baba ake ategeemee hayo! Kama unakaa kwenu ni bora kumfunulia wandani wako jinsi unavyojisikia na kufanyiwa na mkwewe ili amrudishe huko kwake naye akakae na mke wake! akamalizze shida zake huko huko
 

kAMA NI MIMI WALA SIMSHITAKII MUME WANGU WALA NINI NAMVIZIA KWA KUJILENGEHA NA KISU AKITAKA KUNIBAKA TU NAMKATA MAGUDUMONI YAKE HALAFU MUME WANGU MAJIBU ATAPATA LABDA ASISHTAKI AVUMILIE MAUMIVU HADI THE END UNLESS OTHERWISE NAJUA NI LAZIMA ATASEMA TU BALAA LITAPOMKUTA NA NDIPO ATATOA SABABU ZA GARIKA HILO LILILOMKUTA KUA ALIANZIA WAPI MPK YAKAMSIBU NYAMBAF MTU MZIMA HOVYOOOOOOOOOOO.
 

Tamaa ya baadhi ya wanaume mhh!
Hii imenifanya nikumbuke majadiliano hapa JF kuhusu wanaume wanaowasarandia ma hausgeli na kudai ati mama mwenye nyumba anabweteka na ndio maana hausgeli anatembea na mume! Sasa hapa tunaona baba mkwe kaja kufadhiliwa kwa watoto, bila aibu anaanza kumnyemelea mke wa mwanawe! SASA AKINA KAKA/BABA hapa JF mtatuambia nini? Mwanaume mwenzenu anataka kufanyiwa kitu mbaya, mshaurini! Mi sina hata la kusema maana hiki kitendo kinafanywa na wanaume wengi. Nimewahi kushuhudia marafiki wa kiume wakiwataka wake za marafiki zao, nimesikia mkaka akimtaka dada binamu, nimesikia mwanaume akiwataka mashemeji wa kike.... sasa tusubiri akina kaka waje na suluhu kwa hili.
 


uwe makini sheria inaweza chukua mkondo wake kwa maamuzi hayo
 
The Bible says 'a man shall leave his father and mother and be joined to his wife, and they shall become one fresh' Genesis 2:24(The Gidions).

Matatizo ya ndoa nyingi zinatokana na kupuuzia huu mstari. Nashauri sana muache kubebana make ndo chanzo cha matatizo mengi kwenye familia.
 
Kwanza tumuulize huyo mdada huwa anavaaje, anakaaje anapokuwa mbele ya babamkwe? pengine vaa yake au kaa kaa yake mbele ya baba mkwe imekuwa ni mtego kiasi kwamba kaanza yeye kuamsha makasia ya baba mkwe! Tusipende kulaumu wanaume huenda chanzo ni yeye! Je kapita na kanga moja mbele ya mkwewe:A S 8:
 
Kuhama ni uamuzi sahii, mshauri mwenzako haraka.
 
Amweleze kwa lugha ya kidiplomasia, kuwa jamani mume wangu naomba umshauri baba aende nyumbani kwani kwa kuwepo kwake hapa nahisi nitavunjiana naye heshima siku moja... Then asisitize kuishia hapo hapo, ili kuondoa hatari yeyote ya kuwagombanisha... Kama mume ni muelewa atakubali, asipoelewa, ampasulie ukweli, pwaaaaaaaaaaa...
 
uwe makini sheria inaweza chukua mkondo wake kwa maamuzi hayo

naamini itachukua kotekote kwani hata yeye anavunja sheria kwa kunyatia mali ya mwanawe pambaf zake.
 
Amwambie mmewe ili baba arudishwe Moshi haraka iwezekanavyo la sivyo atabakwa.
 
Unauliza majibu? mweleze ukweli wote mume wako ambaye ndio ubavu wako ili ajue. Sasa unataka ajue baada ya kubakwa?Ndio jaribu la awali kwa ndoa yenu.
 
Dawa ni kumwambia mumewe maana hilo ni tatizo kubwa sana,halafu hii tabia ya wazazi kuja kukaa na watoto wao wakati hawajafaidi ndoa yao nayo ni kero kubwa na inatakiwa ikemewe na wote wanaojali ndoa.
Huyo mkwe si akakae na mkewe?Kisa cha kuwanyima raha watoto ni nini?Au ndio kamchezo ka huyo baba kupitia wake za watoto wake?
Huyo baba mkwe FATAKI asilaziwe damu kwani madhara yake ni makubwa baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…