Msaada bei ya hivi vifaa vya ujenzi

Jozen

Member
Joined
Dec 22, 2016
Posts
42
Reaction score
66
Habari wadau kwema? been a while nimekua msomaji tu humu ila leo nimeona nitafute msaada wa kiuzoefu huko nyumbani

Currently naishi mbali na Tanzania na nilikua najaribu kufanya overview ya bei za vifaa kwa sasa maana karibu nije kumaliza kakibanda kangu ka kuunga unga na sasa hizi bei zilivyo chachamaa ndio balaa tupu.

Please kwa mwenye uzoefu kwa bei za vitu vifuatavyo anaweza share.

1. Nondo 12mm per piece
2. Kokoto nyeusi kwenye Ile tipa wanaita mende
3. Zile paving blocks(solid)
4.Mchanga wa plasta tipa (mende)
5. Bei ya PVC kwa sasa
6.Tanga stone

Tujikusanye tukamalize haka kakibanda tukijua uhalisia wa materials.

Ni hayo tu ahsanteni.
 
Mpaka hapo ilipofikia haujui bei halisi ya nondo, kokoto na mchanga....
 
Mkuu unatuchora bana...

Engineer wako yupo wapi?
Mkandarasi sio rafiki niseme kila kitu ni ndio ndio lazima ujilidhishe hasa kama unaishi mbali na Tanzania
 
Mkandarasi sio rafiki niseme kila kitu ni ndio ndio lazima ujilidhishe hasa kama unaishi mbali na Tanzania
Sawa lakini na mtoa mada mawenge, bei zinatofautiana na eneo mtu aliopo. La pili kwanini asiende dukani kuuliza ambapo ni karibu na eneo analojenga wakati maduka yamejaa?
 
Sawa lakini na mtoa mada mawenge, bei zinatofautiana na eneo mtu aliopo. La pili kwanini asiende dukani kuuliza ambapo ni karibu na eneo analojenga wakati maduka yamejaa?
Mtoa Mada sio mawenge mtoa Mada ameuliza akarudia kusema anaish mbali na nchi Kuna shida?
 
Kwani hayo material uliojengea mwanzo ulinunua kwa nani? Kwa nini usimuulize kuwa sasa hivi anauza kwa bei gani
 
Kwani hayo material uliojengea mwanzo ulinunua kwa nani? Kwa nini usimuulize kuwa sasa hivi anauza kwa bei gani
Tatizo ujuaji mwingi sana humu, when one ask Kuna reason behind. Issue ilikua simple tu kuignore au kujibu swali.
Unafikiri siku Consider kutick all the boxes kabla sijauliza.

Fatilia vizuri uzi usikurupuke bwana mdogo
 
Reactions: apk
Hongera mjengo umetulia kabla haujakamilika.... inaonekana ni 🔥🔥
 
1. Nondo 12mm@ 24,000
2. Kokoto 100,000/m³ hadi 110,000 imepanda wiki hii(ilikua 90,00/m³
3. Paving 22,000 zile za kutengenezwa kwa mashine.
4. Mchanga 300,000 hadi 350,000 inategemea maeneo
5. Pvc 200,000m²
6. Tanga stone inaanzia 28,000 mpaka 35,000( bei inategemea quality)
In case kwa kingine nicheki 0752662663
 
Nakutafuta kesho mapema
 
Chief Mie nimependa Mjengo ulivyo.
If possible Naomba Ramani yake
 
Hivi watu sijui wanashida gani ,mtoa mada kauliza swali vizuri tu..ila hizo comment ndo balaa.we all know bei imepanda sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…