Msaada: Biashara ya kutunza hesabu za wafanyabiashara wadogo

Msaada: Biashara ya kutunza hesabu za wafanyabiashara wadogo

ideal

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
109
Reaction score
14
Mimi ni muhitimu wa chuo kikuu ngazi ya degree, nina uzoefu wa uhasibu wa miaka miwili katika kampuni binafsi hapa Geita. Nina lengo la kuanza biashara ya kuwasaidia wafanya biashara wadogo wadogo kutunza hesabu zao. Na kuwawezesha kujua taarifa na riport za bihashara zao kila wiki,mwezi,na mwaka. Mwenye uzoefu wa biashara hii anisaidie na naomba Mawazo ya wadau.
 
Soma vizuri post yako na rekebisha ulipo kosea ilete maana lengwa.
Wazo lako ni zuri hiyo niliwahi kumuona jamaa mmoja msoma anaitwa kaiza, anafanya ulivyo waza, yeye alikua anawatembelea wenye maduka na kuwaelezea anacho fanya, kwamba anawapangia mahesabu mzigo ingia na mauzo kwa wiki na mwezi katika daftari mbili moja ni kwaajiri ya tra wakija na la pili lina data halisi abapo linamuongoza mmiliki ktk kukuza biashara na kukopea bank, ingawa italipa kama utakua na wateja wengi.
 
Mbona naona iko sawa tu @ bab-D kwani wapi haijaeleweka nirekebishe ?
 
OK.....ahsante sana bab-D. Mimi kwa nyongeza natarajia kutumia QuickBooks kuwafanyia hesabu hizo. Sema wafanya biashara baadhi hapa Geita bado ni wabishi na hawataki kubadilika. Jambo la kutunza kumbukumbu za hesabu kwao sio kipaumbele.japo ntapambana kupata Wateja.
 
Last edited by a moderator:
Sorry, (wafanya biashara wadogo.)=wachache au wadogo wadogo.
 
Ahsante namaanisha wafanya biashara wadogo wadogo@bab-D
 
Back
Top Bottom