Msaada: Biashara ya Nyumba ya Wageni (Guest House) imekaaje?

Ifanye iwe classical kwa gud finishing, avoid short time, kua na walau pair tatu za shuka

asee kama uko kwenye mawazo yangu...nataka nikatengeneze kawe kazuri sana ambako mtu atataka aje tena na atoe recomendation kwa watu wengine....vp kuhusu ishu ya mhudumu kusema ameuza vyumba viwili kumbe aliuza sita?
 

lakini vp kaka inalipalipa?mi target yangu ni kupata angalau profit ya 750.000 kwa mwezi.itasaidia kuongezea income ya mshahara. majukumu mengi mkuu na familia inakua...soon watoto wataanza kindergarten na pre school
 

Unaweza Kuifanya Kuwa Hostel Ya Wanafunzi Kama Unaogopa Kuibiwa.Kama Ni Logde Weka Wafanyakazi 5.Mlinzi Wa Usiku Mmoja.Wasichana Wawili Wa Kusafisha.Mmoja Usiku Na Mmoja Asubuhi. Mpokea Wageni Receiption Wawili Mmoja Mchana Na Mwingine Usk.
 
 
Nyamtala Kyono that's peanuts, utapata zaidi ya hapo bila hofu tena na kodi zote za serikali utakuwa umelipa!

My experience: miezi katika ya 3 mpaka 6 unapoianza itakukatisha tamaa! Why? because utakuwa huna "goodwill".

Aidha labda uwe umeitega katika eneo lenye high population. Kuhusu wafanyakazi ningekushauri uwe na watatu (3) kwa kuanzia, yaani 2 receptionists pia wawe wanatandika vitanda, Na 1 mfuaji ambaye pia atakuwa ni cleaner.
 
short sasa ndio hela yenyewe ktk lodge!

Ni biashara nzuri ambayo inaingiza pesa kila siku lakini kurudisha gharama itakuchukua muda kidogo.

Mbaya zaidi ngono zembe inakuwa ni kambi ya michupuko na kuambukizana magonjwa ya zinaa.
 
Mkuu nina uzoefu kidogo na hiyo biashara, kwa vyumba 7 mpaka 8 uwe na wafanyakazi watatu wanatosha kabisa.
Mafanikio ya hiyo biashara inategemea na mahali ilipo na ubora wa huduma pia maana ukilipa kodi, hotel leavy, umeme , maji safi na taka mishahara ya wafanyakazi wako na matumizi mengine madogo kama location mbovu utajuta.
Manispaa wanapiga sana kwenye hotel leavy ambayo ni kila mwezi lazima ulipe na ina deadline.
 
nawashukuru sana kwa michango yenu ngoja niendelee na hii plan ntawapa feedback nikifanikiwa kuanza. location naona sio mbaya. mwanzo niliplan kuwa na wafanyakazi wawili tu ila nimeona watatu ndio watatosha sababu ya rotation. kwa sababu ya uzuri wa vyumba average price nimeona iwe kama 10.000 per room per day
 

Mkuu kwa bei hiyo ya 10,000 kama ni Dar tegemea maumivu,kwasababu zifuatazo:-
  • Biashara hii matumizi ya maji ni makubwa (maji safi/ kunyonya maji taka)
  • Garama za umeme kama itakuwa na AC.
  • Hotel leavy
  • TRA
  • Mishahara ,Sabuni n.k.
Sasa kwa bei ya 10,000 kwa vyumba saba labda kama hiyo sehemu itakuwa kwaajili ya wanaoingia na kutoka. kama ni sehemu ya watu wanaolala hutaiona faida garama za eundeshaji zitakuwa kubwa faida itakuwa ndogo sana.
 

nimekadiria kama ifuatavyo.
kwa siku:
tra........sh.2000
mishahara....15000
umeme....2000
sabuni na maji....5000
emergency....sh 6000

total cost per day....sh 30.000

mapato per day:
kwa vyumba nane ....sh 80.000
occupancy rate nimeweka iwe 70%
hii ni sh. 56.000.

net income per day...56.000-30.000=26.000

kwa mwezi.... 26.000x30=780.000
at the lowest
 

Kwa kifupi kwa mchanganuo wako huo na bei unayopanga kuiweka tegemea hasara au garama utakazotumia kurudi baada ya miaka 10. ni bora uweke hosteli tu, maana hapo matengenezo yatakuwepo kila wakati watu wa afya hawatakuacha utaona garama za uendeshaji kubwa kuliko mapato yako.
 
Camera zipo za satelaiti unaona ukiwa popote eitha nyumbani kwako.resepshn&usafi 1na mlinzi1wanatosha
 
Hiyo kitu ni ngimu Nyumba 10 standard vya guest viwekiwango anatakiwa awe Na 130m. Guest ni kitu ingine kabisa. Return inategemeana Na location ilipo guest napia competitor s wengine
 
Habari wana jamii forum

Nina lodge yangu sass nataka kufanya biashara na watalii. Nimeshauriwa kufanya marketing sasa sijui pa kuanzia, idea ya ku link hasa huko wanakotokea kama mfano kujua mawakala wao nakadhalika. Naomba msaada kwenye mwenye idea ama kujua biashara hii ya utalii.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…