Msaada: Biashara ya Nyumba ya Wageni (Guest House) imekaaje?


Kwa uzoefu wako,watumiaji wengi wako interested na aina gani ya vyumba (self au vya kawaida) au mradi chumba kipo basi.

Nafikiria kuinvest uswahilini ambako hakuna wageni bali wachepukaji tu,self or vya kawaida ndo vitafaa?
 
Kwa uzoefu wako,watumiaji wengi wako interested na aina gani ya vyumba (self au vya kawaida) au mradi chumba kipo basi.

Nafikiria kuinvest uswahilini ambako hakuna wageni bali wachepukaji tu,self or vya kawaida ndo vitafaa?

Watu wanataka SELF Na Viwe Cheap, Usalama Wao Na Privacy I Mean Milango Ya Nyuma Iwepo Ili Wasionekane Sana Na Pia Customer Care Inatakiwa Iwe Nzuri Umpate Mtu Mchangamfu Mwenye Lugha Nzuri.
 
Hata wakij n cheti cha ndoa utathibitishaje kuwa ni chai wakati cheti hakina picha za wanandoa.
 
Mwambie muhudumu kila tukio arekodi kwenye kitabu afu mzoeshe kumshitukiza na mwambie kila tukio utakalolikuta halijarekodiwa hata la fasta litamfukuzisha kazi
 
Achana nayo haikufai hiyo biashara.
Ili upate hela ni mpaka iendeshwe kihunihuni ndio utapata hela yaani namaanisha wale wanaopata hela huwa wanamezea tu kila wakionacho,yaani hata akiona mke wa jirani yake anaingizwa kwenye hiyo guest ananyamaza tu ili asiikose hela.
Ingekuwa ni hotel tena ambayo iko maeneo ya mjini hapo sawa ungepata wateja sahihi ambao ni halali.
 
Niambie ni Biashara gani Halali ambayo hakuna unyonyaji ?

Mfano lile nanasi unalonunua kwa mkulima kwa Tshs 1000/= au shambani mtu ana-bargain kwa Tshs 400/= Je ni halali kumpa huyu mkulima hivyo visenti kwa shughuli aliyofanya kwa miezi kadhaa....

In short dunia ni dog eat dog..., bora huyu ana-provide mandhari ya watu ku-enjoy kitu natural kuliko yule anayewanyangaya nyuki chakula chao na malkia wao na watoto wao tena..., kwa kuwauwa baadhi (eti anajiita mfugaji..., kwani angewaacha wangekufa)!!???
 
Mbali na overheads za kawaida (ambao nadhani unazijua) moja ya gharama kubwa sana nyingine ni ya wadau wa TRA..., ngoja nikupe pdf hapo chini ya hao wadau
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…