Msaada biashara ya Vyakula toka Mbeya/Iringa

lolalola

Senior Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
123
Reaction score
31
Habari zenu
Nataka kuanza biashara kuchukua mazao kutoka mikoa tajwa kuja Dar
Vitu navyofikiri kuchukua ni viazi, vitunguu au nyanya nilikuwa naomba mwenye uzoefu na biashara toka mikoa hiyo anipe ABC zake na jinsi ya kupata soko Dar
 
viazi vitunguu karoti na ndizi hapo poa........ngoja waje wataalam wa ujasiliamali ....
 
Ni biashara nzuri, unachotakiwa kufanya ni kutengeneza network ya masoko ya hayo mazao.Kwa upande wa vitunguu vile vya Raa Mbuyuni ndio vinapendwa dar.Na ni vizuri ukod gari zima ili mazao yako yawahi kufika hasa nyanya
 
Nashukuru ndugu
Raa Mbuyuni ndio wapi tafadhali?
 
Yale maeneo ya Aljazeera hotel ambapo mabasi yanasimaa ili watu wapate huduma ya chakula nk. Ni Ruaha mbuyuni sorry
 
Habari zenu
Nataka kuanza biashara kuchukua mazao kutoka mikoa tajwa kuja Dar
Vitu navyofikiri kuchukua ni viazi, vitunguu au nyanya nilikuwa naomba mwenye uzoefu na biashara toka mikoa hiyo anipe ABC zake na jinsi ya kupata soko Dar

Mazao unayotaka kuanza nayo ni perishable, hivyo ni vizuri uanze na yale yenye lifespan kubwa kama ndio unaanza.
Ukianza na vitunguu maji ni bora zaidi, kisha tafuta karoti,kisha viazi ( ila msimu huu kwa viazi ni noma, unaweza kulia), nyanya za sasa hivi zina bei nzuri kote, yaani shambani na sokoni, kama unaanza, anza na vitunguu.

Ukipata ndizi mshale au mzuzu ni vizuri, hizi zina maisha marefu, za kuiva acha kwanza,pata kwanza uzoefu.

Ukifanikiwa kupata vitunguu swaumu, ni magoli zaidi.
 
Viazi vina tatizo gani mkuu?
 
Viazi vina tatizo gani mkuu?

Huu ni msimu wa kutoa viazi kwa wakulima wengi huko nyanda za juu, yakitokea mafuriko ya viazi, kwa wasio wazoefu ni kilio, bei inaweza shuka ghafla. Ila kwa wazoefu ni wakati mzuri sana, sababu wanajua namna ya kuwalalia wakulima kwa kusingizia soko.

Kiazi kizuri ni cha mwezi wa sita mpaka mwezi wa desemba, hapo wakulima na wafanyabiashara wanatesa mbaya. Low supply high demand, msimu huu ni kinyume, kuna high supply inayofanya kuwe na low demand.

Taratibu mbinu zinaongezeka, hizi chips wanazopark kwenye vinailoni zinaweza kuongeza soko la viazi siku za usoni.
 
Back
Top Bottom