sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,988
- 4,152
Ushauri mzuri. Pia weka utaratibu wa kumwamsha akajisaidie kila baada ya masaa kadhaa.Wala usimchape! Kwa mujibu wa wataalamu hiyo hsli itaisha yenyewe. Cha msingi aepuke kunywa maji au vitu vya majimaji kama soda kabla ya kulala usiku. Ni vigumu kuamini lakini ndiyo itakavyotokea!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha!!!Mbebeshe kobe mgongoni uku akizomewa na watoto wenzake na ataacha
1.Kuanzia saa moja jioni asinywe maji, soda wala vimiminika vingine.
2.Kabla ya kulala hakikisha anaenda kujisaidia.
3.Muamshe kila baada ya masaa mawili.
4.Usimpe vinywaji vyenye "caffeine" usiku kama kahawa, kokoa na pia usimpe maziwa ya chocolate, hivi vinaitwa "bladder irritants".
5.Constipation pia inaweza kusababisha kibofu kubanwa, hivyo hakikisha bowel movement ipo vizuri kwa mtoto.
Usimchape. Ni hali ambayo hata yeye haipendi. Ataacha mwenyewe
Mimi nilikua kikojozi mpaka nilipofika form 3 ndo nikaacha
Tena nilisoma boarding. Ilifika kipindi niliichukia mpaka shule kwasababu nilikua naitwa kikojozi darasaniHahahaha
Duh ,kuna jamaa yangu alikua kama wewe nilimsaidia sana kumsitiri watu wengine wasijue maana alikua ni bedmate lakini ilishindikana ,alijulikana tu ,mwisho wa siku akakubaliana na hali yakeTena nilisoma boarding. Ilifika kipindi niliichukia mpaka shule kwasababu nilikua naitwa kikojozi darasani
To cut short, mkojo ukimbana mchana mpandishe juu ya mti halafu umwambie akojoe. Habari za kujikojolea kitandani zitaishia hapo. Sielewi hili linafanya vipi kazi lakini kwa kila niliyemshauri ilifanikiwa.Ndugu wanabodi,
Kichwa cha habari chahusika.
Nina binti yangu ana miaka kumi sasa lakini anajikojolea sana usiku akilala. Sometimes huwa namchapa sana viboko ili aache lakini haijasaidia, sasa nimemuacha natafakari njia za kumsaidia zaidi. Adhabu yake huwa ni kumlazimisha afue mashuka na nguo zote anazozikojolea.
Nimeona niwashirikishe ndugu zangu labda kuna yeyote aliyefikwa na shida kama hii na akaitafutia ufumbuzi.
Wenu katika kazi. Nisiye na jina humu. Ahsanteni.