Salama wakubwa,nimepata changamoto kwenye gari yangu,nilipeka kwa fundi kucheki shockup za nyuma make nilikua nasikia mguu mmoja wa nyuma haupo sawa,katika kuitoa kuna bolt inayoshika chini ya shockup ilikataa kutoka akaipiga nyundo ikatoka,tatizo tulisahau kutoa battery terminal kuja kuwasha gari taa ya ABS na PARKING BRAKE zikawaka kwenye dashboard,
Fundi akafungua mguu na kukagua na bahati mbaya brake fluid ikamwagika yote na hapa ndipo tatizo lilipoanzia,ametoa upepo miguu yote lkn bado brake nazipata kwa shida