Msaada, Breki zinasumbua

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
879
Reaction score
991
Za Weekend Wandugu,

Naombeni msaada, nina Rav 4 Kill Time wanaziita. Last week nataka kutoka nayo nkagundua klach/breki imekua laini Sana, yaan ukikanyaga mguu wafika mpaka chini hata kama hujakanyaga kwa nguvu.

Nkamuita Fundi akafungua Sijui ndo master ya breki pale mbele kwenye bonet juu ya sterling, akaiosha osha na mafuta ya breki, akarudishia akaweka mafuta mengine, ikarudi kua ngumu so nkatoka, na nkarudi kupaki kama kawa Jioni.

Baada ya hapo sikulitumia kama week hivi, Jana nakuja kutoka nalo ikawa same story, yule fundi kuja akasema yabidi kubadili rubber kwenye master. Nkampa hela nkatoka bila gari. Jioni nkalitest kweli iko ngumu.

Sasa asubuhi hii tena nataka kutoka nayo inakua same story, ukikanyaga mguu wafika mwisho. Fundi asema Ukitaka kuendesha mkono wa kushoto ushikilie Hand Brake ili ikitokea la kutokea wavuta juu.

Msaada wenu naouomba hapa problem yaweza kua nini? Manake fundi kacheki two times but inakua ni temporary solution tu. Safari zingine zahitaji Gari
 
TATIZO kama Hilo nimetoka kurekebisha wiki iliyopita Tu na hiyo ni baada ya mafundi wangu wa Kariakoo/Gerezan kunipiga pesa Kwa kipindi kirefu Sana..
Hatimae jamaa Yangu alinielekeza hapa Temeke hospital kuna mafundi wa ukweli Sana,
Kilichofanyika fundi alinishauri nibadilishe master cylinder housing na piston zake ambayo inafika tsh 80000/=

Nashukuru baada ya kubadilisha sasa mambo ni poa kabisaaa na kumbe TATIZO lilikuwa ni Ile housing ilikuwa imetanuka kiasi kwamba hata uweke Raba mpya na piston zake bado haiwezi kusukuma mafuta sawasawa.
Pia mwambie huyo fundi aangalie brake system nzima ili kuondoa usumbufu
 
Ufumbuzi Ni Kununua Master Ambayo Ikifungwa Tatizo Lote Litakwisha. Kariakoo Utapata Haraka Ingawa Bei Kwa Usahihi Sijui Ila Ushike Angalau Tshs Laki Moja
Maana Nilikwenda Kununua Ya Ford Ranger Ilikuwa Laki Na Nusu
 
Nunua master tuu nyingine yawezekana imechimba
Hawa mafundi wengi wanabahatisha Tu TATIZO nakumbuka suala la silence ya gari imenisumbua takribani mwaka sasa lakini huwezi amini leohii nipo hapa garage na fundi amesharekebisha na gari iko poa kabisa,
Mafundi wengi walikuwa wanahisi pengine ni plug,air filter na muffler kumbe ishu ilikuwa ni tofautiii!!
 
Ufumbuzi Ni Kununua Master Ambayo Ikifungwa Tatizo Lote Litakwisha. Kariakoo Utapata Haraka Ingawa Bei Kwa Usahihi Sijui Ila Ushike Angalau Tshs Laki Moja
Maana Nilikwenda Kununua Ya Ford Ranger Ilikuwa Laki Na Nusu
Carina ti nimenunua Kwa tsh 80000/= na tena fundi alinishauri ninunue used na sio mpya(bei ya mpya iko chini zaidi kuliko used)
Inategemea na Aina ya gari
 
Kariakoo Shauri Moyo Atapata Used Nzuri Sana Wanaokata Magari.
Maeneo Ya Kariakoo Kituo Cha Bakheresa
Pale Maduka Mengi Sana Wanauza New
 
Kariakoo Shauri Moyo Atapata Used Nzuri Sana Wanaokata Magari.
Maeneo Ya Kariakoo Kituo Cha Bakheresa
Pale Maduka Mengi Sana Wanauza New
Nimepaelewa pote ulipopataja Mkuu. Kariakoo naanzia mataa ya Bakhressa pale Sijui ndo fire naambaa ambaa alongside msimbazi road Mpaka Kule mbele kote ni maduka yale.

Otherwise used ni pale opposite Al Haramain au nyuma ya shule ya uhuru. Sema sasa bei ndo nijiandae kupigwa wakiona mdada lazima iwe juu.
 
Kuna barabara ya Tandale Uzuri fund kaniambia napo wanakata spares na bei zao nafuu Ila ndo used za Tanzania,
Siyo Mbaya Ukiwa Na Fundi Wako Atazame Hiyo Used Tanzania IwapoIko Kwenye Hali Nzuri
 
Haa Maeneo Ni Hayo Hayo Ila Biashara Huria Kupigwa Kupo Ila Sasa Ukiwa Na Fundi Wako Unaweza Kuepuka Kupigwa (Kunyooshwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…