I think huwa between july and august. na inaitwa access course. angalua website yao kwa mahitaji
Mkuu, nashukuru kwa mchango wako.
Website yao haina maelezo ya yanayojitosheleza kama muda wa kuanza Access Course, ada, na taratibu zipi zifuatwe ili kusoma hiyo Access Course.
Mkuu, kuna ACCESS (PRE-ENTRY) COURSE, ambayo ni kwa wale waliosoma Certificate/Diploma ya Engineering lakini ufaulu wao haukidhi vigezo vya kujiunga na B.Eng na wataisoma kwa wiki 10 na kuna BRIDGING COURSE kwa wahitimu wa Form VI PCM, PCB, EGM na EGM ambao wataisoma kwa wiki 34. Shida yangu ni kuhusu BRIDGING COURSE. Bado nategemea mchango wako wa mawzo Mkuu.
Mkuu kwa wanafunzi wanao soma B.ENG amabo hawakupitia diploma au FTC wana miaka 4 ya masomo yani 1st year - Unaitwa Bridging course 2nd - NTA level 7 3rd year - NTA level 7B 4th year- NTA level 8 Na kwa masters inaitwa NTA level 9 na PHD inaitwa NTA level 10 Bridging course ni mwaka wako wa kwanza wa masomo kupigwa brush kuhusa maswala ya uhandisi kam Engineering Drawing na masomo ya NTA level 6(mwaka wa mwisho wa diploma) Usipokuwa na vigezo vya bachelor degree huwezi kusoma bridging course mkuu
Nashukuru Mkuu, ila kuna utata, maana kwenye TCU guide book wameandika kuwa ili kusoma B.Eng, katika chuo cha MUST, lazima principle pass moja iwe ya mathematics. Je kwa aliyesoma PCB atawezaje kusoma bridging course ya B.Eng mwaka wa kwanza wakati TCU hawawezi kumchagua kusoma B.Eng hapo MUST? Au kuna kuomba chuoni moja kwa moja? Tafadhali naomba msaada wa ufafanuzi.
Pili, je mtu aliyesoma Diploma in Computing and Information Technology anaweza kuchaguliwa kusoma B.Eng in Computer Engineering? Kwenye guidebook hii program haikuwekwa, lakini kwenye website ya chuo wameiweka, na wanataka aliyesoma Diploma in computer Engineering/science. Naomba ufafanuzi tafadhali.