pole sana mkuu, nimesikia MOMBASA kuna hospita nzuri sana lakini sina uhakika sana, labda subiri majibu utapata tuHabari zenu wanajamvi
Nina kaka yangu ambaye amerudi Dar kutoka Ulaya alipokuwa anaishi, sasa sisi hatufahamu kama anatumia madawa ya kulevya, ameanza kuumwa na kutetemeka na anafanya fujo sana ili apate hayo madawa yake.
nilikuwa naomba msaada wenu, wapi tunaweza kumpeleka apate matibabu ya uhakika
thanx mkuuPole ndugu, mimi pia nina tatizo kama lako. Niliingia humu jamvini nikapata ushauri na maelekezo: Jaribu Muhimbili psychiatric unit, au Tanga (Lutindi Mental Hospital), au Mombasa.
Kwa bahati mbaya bado sijafanikiwa kwani anaendelea kutumia. Labda Kaka yako hajafikia chronic stage, anaweza akafanikiwa kuacha. Nashauri Lutindi ndio panasifika sana.
sumu ya teja ni segerea mpelekeni fasta apone
ushauri wa bure,mtu hawezi kuacha kutumia hayo madawa bila kutaka.Tumieni nguvu ,kutetemeka ni dalili ya dawa kuisha mwilini[wthdraw syndrome],hivyo atakuwa anafujo ile mbaya.Cha kufanya.kaongeeni na polisi,kisha awekwe ndani,hata kwa wiki tatu,halafu baadaye mtoeni.Hiyo sumu itakuwa imeisha.baada ya hapo muanze matibabu ya kisaikolojia.msisahau kumpeleka kwa wala unga chronic awaone walivyochoka.hapo atapata tafsiri ya wapi alikuwa anaelekea.
Mpeleke kwa pusha akajidunge, atapona.