Msaada: Changamoto ya kushindwa kubana mkojo

Kaory

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2022
Posts
537
Reaction score
1,114
Habarini wana afya,

Mimi ni mwanamke umri ni 40+, nina shida kwenye kubana mkojo. Nikibanwa na mkojo nipate haraka mahali pa kujisitiri vinginevyo unatoka kidogokidogo yaani kuubana siwezi au kuvumilia.

Nilishafanyiwa operation 4, mbili za uzazi na mbili za goita, sasa wengi wanasema kwa kuwa nimetumia catheter Mara 4 huwa zina tabia ya kulegeza mishipa ila sina uhakika na hilo.

Kama kuna tiba au ushauri kutoka kwa wataalamu naomba msaada wenu. Asanteni in advance!
 
Una mume au una mahusiano yaliyo hai??........kama jibu ni ndio basi hapo ndio kwenye tiba mjarabu
 
Nakunukuu: ''sasa wengi wanasema kwa kuwa nimetumia catheter Mara 4 huwa zina tabia ya kulegeza mishipa ila sina uhakika na hilo''

Usiwasikilize hao ''wengi wanasema '', Nenda hospital upate msaada immediately
 
Nashukuru kwa ushauri, kesho nitafanya hivyo
 
Jaribu kutumia juice ya miwa au majani ya mlonge
 
Waweza kwenda kwa gyno wako hospital atakushauri ,upo mkoa gani mikushaur Dr mzuri
 
Nenda hospitali wakaangalie tatizo ni nini.
 
Pia nimeona tangazo meli ya wataalamu kutoka China itafanya uchunguzi na gynecologists watakuwepo, nitaenda pia kupima huko
 
Tezi dume hilo. Wahi kwa urologist
 
Nakunukuu: ''sasa wengi wanasema kwa kuwa nimetumia catheter Mara 4 huwa zina tabia ya kulegeza mishipa ila sina uhakika na hilo''

Usiwasikilize hao ''wengi wanasema '', Nenda hospital upate msaada immediately
Sahihi
 
Dr aliwahi kunihudumia kwa shida hiyi ali nishauri kufanya kegel exercise, pia alisema watoa huduma wanapswa kumfahamisha nini cha kufanya baada ya kutolewa catheter ili kuepusha atari hyo, mimi kwa hyo kegel exercise imesaidia nimerudi kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…