Msaada computer inaniumiza kichwa

Jentelomeni

Member
Joined
Aug 21, 2023
Posts
11
Reaction score
64
Habari zenu wataalamu
Nina PC ya HP mara nilipoogeza tu disk zingine zikawa tatu ikawa kila nikiwasha inaniletea maelezo na maelekezo huku ikitaja na majina ya disk na nafasi zilizomo humo

Sasa juzi nikapata muda nikayafatisha jinsi yanavyo elekeza yale maelezo maelezo yenyewe yako kwenye picha hapo mpaka sasa computer yangu haimalizi kuwaka inaishia kwenye maandishi yananichanganya sijui hata nifanyeje
 

Attachments

  • IMG_20240725_201909_992.jpg
    3.3 MB · Views: 4
Picha za juu zinaonesha Disk zipo ila za chini zinaonesha kama kuna Disk error, jaribu kuchomoa na kuchomeka tena hizo Disk zako, ikigoma tena jaribu kuzipeleka kwenye PC nyingine uone kama zitasoma, zikisoma.
piga windows tena.
 
Kuna mawili disk yenye windows inapaswa kuwa ya kwanza, kwenye Boot sequence(hii setting ipo kwenye BIOS) ama pengine settings zako zinahitaji RAID disk na disk zako zimesoma Non RAID, pia setting ipo kwenye BIOS either uweke Legacy au option ingine jaribu kuboot tena.

Kama una uweza kuingia kwenye BIOS basi tupe picha zake pia
 
Kwa kuangalia picha ya BIOS settings uliyoiweka, inavyoonekana BIOS inaonyesha kuwa kuna RAID0 volume inayoitwa "Volume Chifu" ambayo ni bootable. Hii ina maana kwamba mfumo unaweza ku-boot kutoka kwenye diski kama harddisk ina OS.

BIOS Setup
  • RAID Volume
    • ID: 0
    • Name: Volume Chifu
    • Level: RAID0 (Stripe)
    • Size: 357.7GB
    • Status: Normal
    • Bootable: Yes
  • Physical Devices
    • Device 0: SAMSUNG MZ7LN128 (119.2GB)
    • Device 2: ST500DM002-1BD14 (465.7GB)
    • Device 3: ST500DM002-1BD14 (465.7GB)

Nilichokkiona
  1. BIOS Setup
    • BIOS imewekwa vizuri kwa sababu RAID0 volume inaonekana na ina status ya "Normal" na imewekwa kama "Bootable". Hii ina maana BIOS inaweza kutambua na ku-boot kutoka kwa volume hii.
  2. Hard Disk Bootability
    • Kama kuna mfumo wa uendeshaji (OS) kama Windows kwenye hiyo RAID0 volume, basi mfumo unaweza ku-boot vizuri kutoka kwenye hard disk.

Cha kufanya
  1. Hakikisha OS Inafanya kazi
    • Hakikisha kwamba Windows au mfumo mwingine wa uendeshaji umewekwa kwenye hiyo RAID0 volume.
  2. Hakiki Boot Order kama ifo ssawa
    • Ingia kwenye BIOS setings na hazikisha kuwa "Volume Chifu" ipo kwenye nafasi ya kwanza kwenye bout order, ili BIOS ikaribu kuanza kutoka kwenye volume hii kwanza.
  3. Run Diagnostic Tools
    • Kama changamoto itaendelea, basi unaweza ukafanya tools diagnosis yaani usngalie hardware na diski kama chkdsk ili kujua hali ya diski na mfumo mzima wa RAID.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…