Nakuomba tembelea jukwaa la Wajasiriamali huko kuna Nondo za Maana.
Kwa Niaba na shukran za dhati saana kwa MAMA JOE na copy kama ilivyokuja,maana nimeweka kwenye booklet yangu
Nitaanza na ugonjwa wa KIDERI (Newcastle desease).
Hapa mimea mikuu mitatu hutumika sana ambayo ni ALOE VERA, KATANI , MWAROBAINI
Unachukua KATANI MBICHI(ie ya kijani ambayo haijakauka) unatwanga kwenye kinu, maji au ule uji uji wake unaukusanya, unaweka kwenye vyombo safi na unaongeza maji kiasi ili kupata mchanganyiko mzuri, Kwa kuwa ni dawa ya kienyeji haina kipimo maalumu sana, ila unatakiwa ukadirie isiwe kali sana wala isiwe nyepesi sana, cha msingi lile povu povu lake lisipotee, dawa hii ni kinga nzuri sana kwa KIDERI(New Castle). Wape kuku kwenye maji yao ya kunywa angalau kila mwezi SIKU TATU au SIKU NNE mfululizo na ni kwa umri wowote ila wasiwe vifaranga wadogo sana.
· Kama huna KATANI unaweza kutumia ALOEVERA, chukua aloe vera twanga na changanya na maji kidogo ili isiwe kali sana na pia zingatia isiwe nyepesi sana kisha wape hiyo juisi kama maji ya kunywa. Baada ya hapo unakaa kama wiki mbili au tatu unawapa muarobaini.. Lakini hii ni kinga tu sio tiba na haina madhara, ila wakiumwa inabidi ufuata ushauri wa daktari wa mifugo.
ugonjwa wa KUHARA(jina la kizungu nimelikosa)
Kama kuku wako wanaonesha wana ugonjwa wa kuhara na ukajaribu dawa za Madukani na zikashindwa kufua dafu, au wanahara na hujui ni ugonjwa gani kwani kuhara kunaambatana na magojwa chungu nzima, basi dawa hapa ni MAJANI YA MPERA.
· Twanga majani ya MPERA AMBAYO HAYAJAKAUKA na ile juisi yake wawekee kwenye maji, ila kama unataka ifanye kazi vizuri changanya na MUAROBAINI na ALOE VERA, kuku wako watafunga kuhara mara moja na haina madhara yoyote kwani kuku hupenda sana kula majani. Unaweza kuwapa siku nyingi kadiri utakavyo ila ni vizuri ikawa siku tano mfululizo kwa mwezi mmoja.
Note kitu kimoja,
Siku zote madaktari wa mifugo na wanyama wanafurahi sana wakikuta umepanda ALOE VERA, MUAROBAINI na KATANI kwani wanatambua umuhimu wake.
Lakini pia kumbuka kama ilivyo kwa Binadamu usipende kuwapa kuku dozi za hospitali na za kienyeji kwa wakati mmoja, unawageuza miili yao kuwa CHEMISTRY LABOLATORY na kufanya CHEMICAL REACTIONS. Kama umeamua kuwapa dawa za madukani sitisha za kienyeji mpaka watakapo maliza za madukani, kama umeamua kuwapa za kienyeji vivyo hivyo sitisha za madukani.
Nitaendelea na magonjwa mengine na tiba zake mbadala kadri ninavyozidi kuzinyaka.