Msaada; Duka la Clarks Kariakoo lipo maeneo gani?

Msaada; Duka la Clarks Kariakoo lipo maeneo gani?

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Ndugu watanashati,

Kuna duka la Wahindi walijitanabaisha kama wakala wa clarks—walikuwa wanauza viatu vya brand hii pale Dar es Salaam jirani na mnazi mmoja. Huwezi amini ni mahali nimeshafika lakini huwa nashindwa kupakariri(nina tatizo la kisaikolojia kuhusu kushika maeneo).

Penyewe ukitoka Mnazi mmoja unakuwa kama unakwenda Kitumbini.Kuna ule mtaa wanauza vitenge.Kisha unafanya kama unataka kwenda msikiti wa Kitumbini. Sasa ninaona nyota tu hapa. Ninapoteza ramani kabisa. Sipaoni jamani Nimeuliza wadau hapa ni kama hawanielewi.

Ni jamaa wa kitambo sana kabla hata ya ujio wa bidhaa duni za kichinachina.Nje wamebandila kibao kabisa Clarks.

Ninauliza kubahatisha hapa penye wengi,ukute kuna mtu hapo ni uwanja wa nyumbani anielekeze.

Ninawasilisha
 
Back
Top Bottom