Msaada:Elimu kuhusu Group of Companies hapa Tanzania.

Msaada:Elimu kuhusu Group of Companies hapa Tanzania.

melech

Member
Joined
May 29, 2013
Posts
62
Reaction score
25
Kwanza, shukrani kwa wale wote ambao huwa wanatumia jukwaa hili kutuelimisha sote kuhusu masuala haya ya uchumi. Bila shaka kwa kufanya hivyo JamiiForum imekuwa njia ya wengi wetu kupata elimu/maelekezo/msaada kwa ajili ya mambo yahusuyo uchumi wetu na taifa pia. Mungu awabariki.

Mimi naomba mnisaidie elimu (na maelekezo) kuhusu kuwa na Group of Companies hapa Tanzania. In the future, nina imani na nia ya kuwa na makampuni kadhaa yanayojishuhulisha na mambo tofautitofauti. Sasa kuna kitu huwa ninajiuliza, hapa natakiwa nifanye nini, nisajili kampuni moja ambayo itafanya mambo yote hayo? Ila huwa nadhani ni vyema kuwa na group of companies, ambamo ndani yake/itajumuisha makampuni tofautitofauti kila moja na shuhuli zake tofauti.

Sasa hapo ndio ninaomba elimu zaidi, kampuni moja yenye kufanya mambo yote hayo au group of companies?
  • Zipi faida za kila mojawapo ya options hizi?
  • Zipi changamoto zao?
  • Kwa mipango niliyoileza hapo juu, option ipi ni nzuri zaidi?

Nimeshasoma hii https://www.jamiiforums.com/busines...i-katika-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania.html lakini sijaona hizi habari humo. Nasikitika kuwa kwenye website ya BRELA pages za "Companies" na "Business Names" hazina chochote. Niliwahi pia kuwaandikia e-mail na hawajawahi kunijibu hadi leo!

Thanks in advance.
 
Back
Top Bottom