Msaada: Fedha ya faini ikipatikana inaweza kubatilisha kifungo kilichoanza kutumikiwa?

Msaada: Fedha ya faini ikipatikana inaweza kubatilisha kifungo kilichoanza kutumikiwa?

Night shadow

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
574
Reaction score
1,098
Habari zenu ndugu zangu Naomba kujua pale mtu anapo shitakiwa na mahakama ikamtia hatiani kisha ikamtaka kulipa faini au kwenda jela kwa kipindi fulani.

Je mtu huyo anapokosa hela ya faini nakwenda jela, je ndugu badae watapopata hela hiyo wanaweza kwenda kulipa na akatoka au ni vipi?

Na kuna muda maalumu ambao kama atakaa jela hataruhusiwa?
 
Sina hakika lakini nadhani utachagua adhabu moja kati ya hizo mbili
ukichagua kulipa faini basi utasubiriwa ulipe faini
Ukichagua kifungo utafungwa tu hata kama baadae utakuwa na hela zaidi ya hukumu ya mahakama.
 
Asante,nimekuelewa ngoja tusubiri na mawazo ya wengine
 
Sibu sahihi ni hili hapa, siku yoyote akipata faini Ndugu wataenda mahakamani kulipa watapewa risiti ambayo nyuma ya risiti itagongwa muhuri wa hakimu, halafu Ndugu wataenda na hiyo risiti gerezani watamtoa mfungwa na kuachiwa
 
cha kuongezea ni kwamba hakuna muda maalum wa kumtoa mtu gerezani kwa kilipa faini. Kama imepita miezi kdhaa anaweza kulipa faini gerezani wakapiga hesabu muda aliotumikia hela inapungua.
 
Back
Top Bottom