moto2012
JF-Expert Member
- Jul 3, 2012
- 2,271
- 1,493
Dada yangu ni fundi sanifu maabara (Lab. technician) katika hospitali ya Wilaya X, miezi sita iliyopita aligundulika kuwa na TB, alitibiwa na kupona, baada ya hapo alichukua hatua ya kudai fidia ya kupata ugonjwa akiwa kazini. Alipomwandikia barua Mkuu wake kutaka fidia, alijibiwa kwa kuwa anaishi na VVU hawezi kulipwa fidia. Wadau naomba nisaidieni (hasa wajuzi wa occupational health na occupational laws), je ni kweli dada yangu hastahili fidia? Na kama ndio huo sio unyanyapaa?