kama mdau alivyozungumza hapo juu, TB na HIV ni mtu na binamu yake. TB humtokea mtu pale kinga ya mwili inapokuwa imepungua. maana yake ni kuwa katika mazingira yetu haya, wengi wetu tunatembea ama tunaishi na vimelea vya TB, ila kwa kuwa kinga zetu zipo juu, tunafaidika kutopata ugonjwa huu. pale kinga ya mwili inapopungua, ndipo ugonjwa huu unajitokeza. Katika stages za WHO kuhusu watu wanaoishi na HIV/AIDS, mtu akipata TB anaonesha kuwa yuppo katika stage ya 3 ya kuishi na virusi.
Kwa hiyo ndugu yangu, hapo hakuna fidia. atumie dawa kama alivyoagizwa na daktari, hadi miezi hiyo yote iishe. Mungu atambariki