Msaada Friji lina miezi 3 ila sasa haligandishi

Msaada Friji lina miezi 3 ila sasa haligandishi

BARADIGE

Member
Joined
May 22, 2014
Posts
70
Reaction score
32
Habari za muda huu, ni matumaini yangu mwaka umeanza salama.

Bila kupoteza muda, ninaomba kwa wenye ufahamu kuhusu suala langu. Nina friji jipya kabisa la kampuni ya AILYONS, nililinunua mwezi wa 10. Mwanzo halikuwa na shida yoyote, lakini sasa linashindwa kuendelea na kazi yake kwa muda mrefu—linaweza kuwasha kwa masaa 8 kisha maji yanakuwa na hali ya kawaida, kama vile umeliweka kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Freezer, hakuna kilichooza.

Swali langu ni; Je, gesi inaweza kumalizika kwa kipindi kifupi kama hiki au kuna tatizo lingine?

Pia, kuhusu utaratibu wa WARRANTY, je, naweza kurudisha friji kwa kampuni ili wanibadilishie?

Maana sielewi, bado nipo njiani panda. Natanguliza shukrani.
 
Ailyons au LYONS
IMG_20241231_072957_777.jpg
 
Naelewa kuna kutafuta unafuu wa bei ila hiyo brand siyo Mkuu.

Huo muda ni mfupi sana kutokea changamoto, wasiliana na muuzaji akutatulie hiyo changamoto yako.
 
Mkuu hiyo brand sio umepotea cha kufanya wanaservice center yao pale kituo cha Gold star Dsm watakurebishia fasta. Fika Gold star uliza service yao utaonyeshwa wanaweza tuma mafundi nyumbani wakarekebisha
 
Umefeli hapo kwenye hiyo kampuni AILYONS. Wanatoa products bora liende kwa bei rahisi mpaka zinaogopesha
 
Naelewa kuna kutafuta unafuu wa bei ila hiyo brand siyo Mkuu.

Huo muda ni mfupi sana kutokea changamoto, wasiliana na muuzaji akutatulie hiyo changamoto yako.
Asante ngoja nifanye hivyo
 
Mkuu hiyo brand sio umepotea cha kufanya wanaservice center yao pale kituo cha Gold star Dsm watakurebishia fasta. Fika Gold star uliza service yao utaonyeshwa wanaweza tuma mafundi nyumbani wakarekebisl

Mkuu hiyo brand sio umepotea cha kufanya wanaservice center yao pale kituo cha Gold star Dsm watakurebishia fasta. Fika Gold star uliza service yao utaonyeshwa wanaweza tuma mafundi nyumbani wakarekebisha
Leo nimepeleka nasubr kesho nilifate nione kama Kuna tofauti
 
Nilinunua TV ya Ailyons kuja nyumbani nilivyoona kwamba ni Made in Tanzania nikakosa amani ya moyo kabisa, nikajisemea hapa kitaumana muda wowote. Mpaka sasa ni mwezi umepita ipo vizuri mno.

Kwa case yako jua kwamba hiyo friji ni Made in Tanzania, nahisi majibu umeyapata
 
Back
Top Bottom