Msaada. Garage za wachina, Dar

Msaada. Garage za wachina, Dar

Kisaka80

Senior Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
151
Reaction score
94
Wapendwa wana JF,

Nimewahi kusikia kwamba kwa DSM kuna garage nzuri sana za wachina. Nasikia wapo makini katika kutengeneza au kurekebisha gari na endapo gari ikapata hitilafu then ukaipeleka katika garage zao nasikia gari inakuwa almost new brand.....namaanisha kuwa 'nasikia gari inarudi katika ubora wake wa hali ya juu'.

Sasa kwa yeyote anayefahamu garage za wachina zilipo kwa hapa DSM naomba anifahamishe ni maeneo gani nitawapata.

Mafundi wa kibongo ni wazuri, lakini mimi kwa safari hii nataka gari yangu nijaribu kuwapelekea hawa wachina labda nitapata kutatua tatizo la gari yangu na itakuwa ipo katika standard ninayoitaka.

NB: Je TOYOTA DEALERS......DSM garage yao ipo wapi? na wao je kwa anayefahamu hawa jamaa nao ubora wao katika kurekebisha magari yapoje?

Natanguliza shukrani kwa michango na maoni yenu. Gari yangu ni Toyota RAV4 Kill time.....na sijaifanyia service kubwa toka niinunue mwaka 2009.
 
Gereji zipo ila wanabadilisha mabati hawanyooshi. Tunapishana nao kwenye used. Kazi wanafanya vijana wetu.
 
Usijisumbue kwenda huko kwani wanachofanya wao kama ni bumper la mbele limeumia wanalitoa lote na kuweka lingine na kupiga rangi tuu huwa hawanyooshi ndio maana bei zao zinakuwa zimechangamka kidogo na kazi huwa wanafanya wabongo
 
Mkuu ni heri ukaenda kwa mafundi wa kibongo wachina wana bei kubwa vilevile gereji kama spring city iliyopo mikocheni barabara ya rose garden walikuwa na kashfa kwamba unapowaachia gari lako apart from kutengeneza wataangalia lina parts gani ambazo bado zina hali nzuri na ambazo wakizitoa huwezi shtuka! then wanazitoa then wanakuwekea kanyanga! hili liliwahi kumkuta jamaa mmoja bahati nzuri jamaa gari lake analijua ka anavyomjua mkewe mbona aliwasha moto ikabidi wachina wakubali yaishe! lakini kumbuka hii ilikuwa zamani labda baadae walijirekebisha.... sijui....

Gereji nzuri za wabongo zipo nyingi nadhani Lege, Mshana na wengine wakiona post yako watakusaidia zaidi ila hakikisha kama kuna parts za kureplace sisitiza OG aka jenuini!

Vilevile mafundi wa Toyota weekend wanafanyaga kazi zao private so kama ukipata mmoja itakuwa poa vilevile! maana hapo watakufanyia bei zetu tulizozoea na wala hazina VAT wala 5% withholding tax!!!! na vilevile parts kadhaa atatoa hukohuko Toyota upo hapoooo!
 
Back
Top Bottom