Msaada: Gari haina nguvu

upeo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
369
Reaction score
218
Wakuu habari za majukumu,

Naomba msaada nina Suzuki Kei tatizo lake ni unapoendesha haina nguvu kabisa lakini ukirudisha reverse inakubali na ina nguvu vizuri tu.

Je, wakuu hapo tatizo nini? Nipo Dodoma lakini mafundi kama watatu wananambia ni gia box. Je, wakuu ni sawa?

Naomba msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatumia Transmission Control Unit? Mimi wa nne. Ni transmission hiyo

Sent from my SM-G975F using Tapatalk
 
Ninayo yangu ilikuwa unasumbua hivyoo hivyoo. Kabadilishe coil/plug. Zitakua zinafanya mbili.

Unywaji wa mafuta ukoje??
 
ni kweli gear box suzuki swift na kei ugonjwa gear box ni tatizo sana.jaribu kufungua sample
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni hili, seal ndani ya gearbox zimekauka/kusinyaa na hivyo zinaruhusu pressure ya gear box oil ipotee. Ila je ni maual au auto, maana hii niliyokupa ni kwa auto, simple solution badili gearbox
 
Ni auto mkuu. kina fundi leo kaichafua gia box kasema tatizo ni clauch za mbele zimelika zimefanya kama kuungua hivi kwa hivyo kasema tubadilishe.. Vipi wakuu linawezekana hilo..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…