Mrejesho,
Nimenunua ECU nyengine, bahati nzuri sana mwenyewe amekubali niirudishe ikiwa haijanifaa. Nimeipachika hio ECU, yani hata engine haijawashwa, tukasema tuipime kwanza ECU ina cde gani, tukakuta in Code 12 RPM signal na Code 14. Tukajua kuwa haitowaka gari lakini tukasema tuombe Mungu, tukajaribu ndio ilikuwa inapiga chafya tu ngoma haiwaki. ECU ya zamani nikiweka moto mmoja tu inawaka sema ndio inakata. Tumeamua kuwa ECU sio Tatizo na nimerudisha.
Kilichonikwaza ni mafundi wangu, Walikuja wakanambia kuwa niwaongezee dau, wataiwasha gari kwa kutumia ECU hio hio na wiring hio hio! Ndani ya nafsi nikawa najisemea kuwa hawa tatizo wameshalijua, mda tu, ila wametaka hii kazi niione ngumu na nikubali kuwaongezea hela. Nikapatana nao kidogo, wakanambia watanijibu kesho.