Msaada gari langu

Msaada gari langu

Musasa

Member
Joined
Sep 7, 2010
Posts
23
Reaction score
6
Ijumaa wiki iliyopita nilipeleka gari langu aina ya TOYOTA SPACIO(old model) kwa fundi ili kubadili CV joints maana zilikuwa zinapiga kelele. Baada ya kazi nilikabidhiwa gari langu lakini nilipoendesha kama kilometa moja hivi, break zikawa ngumu sana nikalazimika kusima kwa kutumia hand break. Nikalikokota taratibu kurudi kwa fundi. Tukaenda kwa fundi mwingine ‘mtaalam’ wa magari ya automatic. Akadai kuwa inunuliwe ABS motor nyingine. Ikanunuliwa ya kwanza, tatizo liko palepale. Tukajaribu motor nyingine bado. Tafadhali naomba ushauri kwa aliyewahi kupatwa na tatizo hili, au kama kuna fundi mzuri.
 
Duhh,Yani hadi Mtaalam wa magari hayo kashindwa kutatua tatizo na kukutia hasara ya kununua kifa kingine?
Basi gari hilo pelekea kwa Manyaunyau,litakuwa limerogwa hilo.Au ulibeba mke wa mtu.
We nenda Gerage waulize mafundi wakongwe ,je jamani hivi kweli gari huwa linarogwa?atakuambia ndio na mganga watakupa hapo hapo.
Subiri mafundi wengine wanakuja humu
 
Sina uhakika kama ni ABS motor,nahisi hakuweza kutoa upepo kwenye hizo break uku akipunguza na kuongeza mafuta ya break.
 
Back
Top Bottom