marisi schwein
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 1,037
- 3,146
Gari ni Mercedes C200 Kompressor w204 inaandika autolamp function inoperative.
Tatizo litakuwa ni nini?
Tatizo litakuwa ni nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpelekee mwenye nayo jombaa,kifupi irudishe kwa shemeji yako anafundi wake.Gari ni Mercedes C200 Kompressor w204
Asante ndugu kwa ushauri wako muruaMpelekee mwenye nayo jombaa,kifupi irudishe kwa shemeji yako anafundi wake.
Unajua auto lamp ni nini? Ni ile function ya taa kujiwasha au kujizima kutegemea na mwanga uliopo. Hapo sasa hio function haifanyi kazi. Ni kwamba sensor yake ina tatizo.Gari ni Mercedes C200 Kompressor w204 inaandika autolamp function inoperative. Tatizo litakuwa ni nini?
Kuna kakitu fulani kamekukwama kooni.Mpelekee mwenye nayo jombaa,kifupi irudishe kwa shemeji yako anafundi wake.
Tangu lini we dada
Asante sana mkuuUnajua auto lamp ni nini? Ni ile function ya taa kujiwasha au kujizima kutegemea na mwanga uliopo. Hapo sasa hio function haifanyi kazi. Ni kwamba sensor yake ina tatizo.
Haizuii taa kuwaka,set manual tu uwe unawasha mwenyewe mpaka ukirekebisha hio sensor.
Asante sana mkuuKiongozi
Hongera sana kwa Kumiliki hiyo kitu,
Kwanza nikutoe wasiwasi kuwa sio taitizo kubwa; Kilicho haribika hapo ni Automatic mode ya taa na Wiper
Ukipata hiyo message;
1. Taa hazita weza kujipunguza kwenda Low zenyewe
2. Wiper haitajiwasha yenyewe Mvua ikinyesha
3. Taa hazitajiwasha zenyewe mwanga ukipungua
Maana yake ni kuwa;
Hivyo vitu vitafanya kazi bila shida kwa Kuvi operate manually hivyo endelea tu kuendesha bila wasiwasi kwa kuoperate manually hadi utakapo tengeneza.
Matengenezo yake;
Hako ka sensor kapo hapo mbele kwa driver kwa juu ya kile kioo cha katikati. Kama umtundu unaweza kukachomoa hapo na kuangalia namba zake (zinakuwa kwa mfumo huu A204 870 47 26.); ukizipata unaweza kuagiza au umpe mtu akuagizie (sio ghali) kakija unakapachika au unatafuta fundi akuwekee.
Muhimu: kwa magari ya high end kama Benz, Usiagize spare bila kuwa na namba ya spare parts (kwani huwa haziingiliani)