Msaada: Gharama kwenye ununuzi wa nyumba

Msaada: Gharama kwenye ununuzi wa nyumba

Joined
Jul 18, 2020
Posts
14
Reaction score
11
Naomba kujua ukinunua nyumba, zile garama zinazotumika kuandaa nyaraka au kumlipa mwanasheria zinajumlishwa kwenye gharama za ununuzi au ni matumizi gani?
 
zile garama zinazotumika kuandaa nyaraka au kumlipa mwanasheria zinajumlishwa kwenye gharama za ununuzi au ni matumizi gani?
Hapana, Hazijulishi kwenye gharama za manunuzi.

Hizi ni gharama za ziada zinazobebwa na mnunuzi kama sehemu ya mchakato wa kisheria wa kununua nyumba.
 
Kiukawaida gharama za ununuzi wa nyumba hazihusishi gharama za mawakili wanaoandaa nyaraka na kusimamia mchakato mzima lakini pia hazihusishi mchakato wa uhamishaji umiliki kwenda kwa mmiliki mpa. Lakini endapo utataka hilo kuweza kuhusisha na gharama nyinginezo zozote yaani huduma ya wakili na mchakato wote wa uhamishaji wa umiliki basi ni vema kabla ya mauziano mkakubaliana na muuzaji na kuweka wazi gharama zote za huduma ya wakili na kuhamisha nyaraka zikatajwa katika mkataba wa manunuzi lakini hakikisha kuwa mchanganuo wake unakua wazi ili zisihusishwe wakati wa ukadiriaji ama upigaji hesabu za masuala ya kikodi ambayo hufanywa na TRA an mamlaka za ardi kwa kuangalia mkataba husika.​
 
Jibu rahisi: Ni maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi. Ingawa asilimia kubwa ya mauziano ya nyumba huwa hayahusishi gharama za pembeni. Kwasababu gharama zenyewe sio fixed amount.
 
Back
Top Bottom