Msaada: Gharama za kukodisha Saloon Car na Truck ndogo kwa makampuni au mahoteli

Msaada: Gharama za kukodisha Saloon Car na Truck ndogo kwa makampuni au mahoteli

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari zenu wanaJF,

Katika jukwa hili siku za nyuma pamekuwepo na mada mbalimbali kuhusu kukodisha au kukodishwa Magari Saloon, Truck ndogo mfano Suzuki Cary kwa ajili ya kufanyia biashara.

Katika hizo mada watu walitoa uzoefu wao kuhusu viwango vya malipo ya kukodisha/kukodishwa Saloon Car na Truck ndogo ambapo ilionekana viwango vya Saloon kwa wiki ilikuwa kati ya Shilingi 80,000 hadi 120,000 na kwa Truck ndogo viwando kwa wiki vilikuwa kati ya Shilingi 110,000 hadi 130,000.

Katika mada hizo hivi viwango tajwa hapo juu vilikuwa kwa makubaliano ya kukodisha kwa watu binafsi i.e. mwenye gari anamtafuta dereva binafsi halafu wanaingia mkataba.

Sasa leo naomba kwa wale wenye uzoefu wa kukodisha Saloon Car na Truck ndogo kwa makampuni au mahotel watupatie viwango vya malipo vikoje na changamoto kama zipo.

Nawakilisha

 
Back
Top Bottom