Matendo Andrew
JF-Expert Member
- Apr 1, 2014
- 748
- 367
Nikihitaji kuvusha gari taka Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutembelea kwa mwezi mmoja utaratibu upoje na gharama zake?
Msaada wakuu. Asante.
Msaada wakuu. Asante.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa zanzibar bora ukodi tu tax,itakamatwa mpaka itoke mwezi,watataka uthibitisho kuwa umekuja kutembea na sio kuliuzaUtaratibu ni kwamba inaruhusika,na utapewa kibali cha muda kama sikosei ni miezi mitatu tu.
Na wala hautalipia Tax kama gari nyingine ambazo zinavushwa Dar moja kwa moja na kusalia huko.
Ila Number za Zanzibar ndio utakazo zitumia.
Hapo unalipia tu,Usafiri wa Meli ya Kuvusha na TRA ili kupata kibali,maana ukikamatwa na Majembe watakuzingua tu,halafu pia Traffic ili upewe Permit maalum.
Maana hilo hata wa South Africa wengi wanakuja na Gari zao wale walio kwenye Overland trips na hata wakenya wengi sana wanakuja na Gari zao Dar na kugeuza nazo.
Ila zaidi kama una ndugu Dar mwambie aende TRA na Traffic makao makuu atapewa muongozo ili ajue aanzie wapi.
Hahahaha,hili nalo ni tatizo.Kwa zanzibar bora ukodi tu tax,itakamatwa mpaka itoke mwezi,watataka uthibitisho kuwa umekuja kutembea na sio kuliuza
Ni wamajeshi tu ndio wanaweza kuvuka nayo