Utaratibu ni kwamba inaruhusika,na utapewa kibali cha muda kama sikosei ni miezi mitatu tu.
Na wala hautalipia Tax kama gari nyingine ambazo zinavushwa Dar moja kwa moja na kusalia huko.
Ila Number za Zanzibar ndio utakazo zitumia.
Hapo unalipia tu,Usafiri wa Meli ya Kuvusha na TRA ili kupata kibali,maana ukikamatwa na Majembe watakuzingua tu,halafu pia Traffic ili upewe Permit maalum.
Maana hilo hata wa South Africa wengi wanakuja na Gari zao wale walio kwenye Overland trips na hata wakenya wengi sana wanakuja na Gari zao Dar na kugeuza nazo.
Ila zaidi kama una ndugu Dar mwambie aende TRA na Traffic makao makuu atapewa muongozo ili ajue aanzie wapi.