Ukweli hata mimi nahitaji sana kujua kuhusu utozaji wa gharama za umeme wa Tanesco.
Maana kuna wanaolipa fedha nyingi, na wengine wanalipa kidogo kwa matumizi yanayofanana.
Tujuzeni kuhusu haya magroup ya tariff.
Nasubiri mwenye ubinadamu aje atoe elimu fupi.
Asee kwakweli umeme huu nitatizo kubwa sana sisi imelazimika tutumie umeme usiku tu mchana mzima tunazima menswech nabado tunalipa uwastani wa 140000 kwa mwezi na hapo nyuma tulikuwa tunatumia umeme wa shilingi 30000 kwamwezi, nyumbani hatuna chochote zaidi ya freji2 na TV2. zaid ya hapo ni mapangaboi tumelalamika Tanesco wanadai gharama zimepand hakuna hitilaf ya mita. sijui hili tatizo ni letu tu au kunawengine wanalo
Mkuu hiyo kwenye nyekundu kwa matumizi uliyotaja haiwezekani kabisaaaaaaaaaaaaaaaa! Utafikiri una kiwanda? Au nyumba ni ya wapangaji wengi na kuna wanaotumia umeme umeme kufanyia welding wakati wa mchana mkiwa kazini? Au Kuna mpangaji ana kijibwawa cha samaki (Aquarium)?. Mimi napikia umeme, nachemshia maji birika la umeme, natumia pasoi ya meme, friji iko on masaa 24, TV iko on almost masaa 16 kwa siku, taa 4 (tube light) zinawaka kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi na bill yetu kwa mwezi haizidi 50,000. Kama ni kweli na unatumia mita za Tanesco kuja kusoma kila mwezi, fanya mpango fasta ufunge LUKU.